Hivi wenyeji hasa wa huko Zanziba ni kabila gani hasa na wanaongea kilugha gani..?
Wenyeji wa Wazanzibar ni mkusanyiko wa Makabila tafauti yanayotoka pembezoni mwa bahari ya hindi,na sehemu nyingine hasa bara la Asia
Makabila kama Wasegeju, Wadigo, Wazaramu, Wagunya(hawa wanatokea kisiwa cha Lamu, Kenya).. nk, ndio makabila ya mwanzo kuhamia Zanzibar
Unatakiwa ujue kuwa Zanzibar ilikuwa Empire, Sultani wa Zanzibar ndio walioifanya Zanzibar iwe imetawala ardhi kubwa kutoka Kismayuu, Kilwa mpaka Congo na sehemu nyingine..
Kuna baadhi ya makabila yamekuwa Zanzibar kutokana na ujio WA Sultani Zanzibar, mfano kabla la WAYAO, hawa ni watu wa kusini Tanganyika, hawa watu walifika Zanzibar na msafara wa Sultan alipohamia visiwani Zenji
Kila kabila lina historian yake ya kuja Zanzibar, WADIGO, WASEGEJU, WAZARAMO hawa ni wavuvi walikuwa na utamaduni wa kupiga kambi(dago),..kando kando ya visiwani
WARABU wa Oman, hawa walikuwa wafanya biashara, walifanya makaazi yao Kilwa, baada Waajemi kushindwa nguvu na Wareno..
Wazanzibari baada ya kuona Mreno anatishia kuichukua Zanzibar, Wenyeji wa Zanzibar ambao wakati huo watu wake walikuwa ni mchangangiko wa makabila tafauti ya Afrika na nje ya Afrika waliomba nguvu za kulindwa kwa kumuogopa Mreno, kutoka kwa Sultani wa Oman, Huo ndio ukawa mwanzo wa utawala wa Masultani Zanzibar
WANYAMWEZI hili kabila limeletwa na Sultan, hawa ni watu WAAMINIFU SANA, hili kabila walikuwa ni walinzi wa Sultani, jeshi la Sultani
WASUKUMA hili kabila ni la wachapa kazi, mpaka hii Leo wafanyakazi wengi wa mashambani kule Zanzibar ni WASUKUMA..
WAMANYEMA hili kabila limechanganya damu na Masultani wa Zanzibar, wanawake wa hili kabila walipendwa sana na Warabu, waliwaowa na kuzaa nao..
Pichani ni Sultani wa 13 wa Zanzibar Humoud bin Said, mama ake alikuwa Mmanyema
l
WAHINDI hawa watu waliletwa na Sultani kuja kujenga Zanzibar, mji mkongwe ulijengwa na WAHINDI, milango ya Zanzibar door ni kazi ya Wahindi..
WAIRANI(waajemi) hawa walikuwa wafanya biashara, vile vile walishawahi kutawala sehemu kama KILWA
WAYEMEN (kina Bakharesa) hawa ni sawa na Wairani walikuwa wafanya biashara, vile vile wana historia ya kukaa KILWA..
Mchangangiko wa Makabila ya kiafrika na yale yaliyotoka nje ya Afrika ndio umeunda utamaduni wa KISWAHILI,..
Wenyeji wa Zanzibar wanazungumza Kiswahili tu, wameshasahau lugha za babu zao, kwani haya mambo yalifanyika zaidi ya miaka Mia saba(700)..iiyopita
ZANZIBAR unaweza kuifananisha na MAREKANI, hizi nchi mbili zina mambo mengi yaliyofanana,..
Mfano, Wageni waliohamia Marekani waliunda taifa Lao, wakatengeneza utamaduni na mila zao, taifa la Marekani likaundwa
TRUMP haijinasibu kuwa yeye ni Mskotish, ijapokuwa wazazi wake wanachimbuko la Scotland, America Hivi sasa ni taifa Kubwa lenye nguvu Duniani..
WAZANZIBARI wanatakiwa waige mfano wa WAMAREKANI, waungane wasimamie Taifa lao, wasikubali kubaguliwa au kutenganishwa, kwani wao sio WARABU, sio WAHINDI,sio WAMANYEMA, sio WADIGO sio WAZIGUWA , sio WAZARAMO, nk wao ni Wazanzibari, wana mila na tamaduni zao
Hiyo ni historia fupi ya Zanzibar na watu wake..