Watanzania wenzangu, naomba tutumie uzi huu kumtukuza Sana Mungu kwa kutuponya na kutulinda na corona. Tumponde na kumzomea Sana shetani na corona yake.
Maneno Kama: Corona kwa Tanzania inayomtegemea Mungu imekula wa chuya!
Tuwazomee mawakala wa Corona wanaotaka kuitumia corona Kama mtaji wa kisiasa!
Tutumie uzi huu kumwinua na kumtukuza Sana Mungu, maneno Kama: Mungu wetu ana nguvu kuliko korona!! Mungu
Wetu aliyetuponya na corona mwaka 2020 atatuponya pia 2021!
Kwa Mungu hakuna kisichowezekana, corona ni nini mbele ya Mungu aliyeumba mbingu na nchi!! Tutumie uzi huu pia kumwombea na kumtia moyo Rais wetu Dr John Pombe Magufuli. Namshukuru Mungu kwa kutupa Magufuli mcha Mungu kuwa Rais wetu!!
Asante Sana Rais wetu kwa kutuongoza vema kwenye Vita hii dhidi ya Corona: You are very smart kwa kuipambanisha corona na Mungu!
Pamoja na Mungu ushindi ni hakika! Asante Rais wetu kwa kudharau vitisho vyao, usiwasikilize, Bwana wa mabwana atawanyamazisha!! Usiogope Vita Ni vya Bwana!
Tunakupenda Rais wetu! I can't imagine ingekuwaje tungekuwa na Rais mwoga kipindi hiki!! Au kama tungekuwa na Rais ambaye Ni kibaraka wa makaburu!
Mungu akulinde Rais wetu na akupe maisha marefu!
Pamoja na Bwana Tanzania tutavuka!