Rais Magufuli: Watendaji wangu wananichelewesha. Naomba chama changu CCM kinisaidie kuwasukuma, tumechelewa!

Rais Magufuli: Watendaji wangu wananichelewesha. Naomba chama changu CCM kinisaidie kuwasukuma, tumechelewa!

Yaani aliamua kupitisha kwa force wabunge wAtakaoperform kulingana na matakwa yake Leo anajifanya hakuwaona?? Ujivetie mwenyewe halafu ushangae matokeoo ya vetting yako??
 
Kwanini anapenda kusukuma badala ya kukaa na kujadili njia sahihi ambazo kila mmoja atajisikia huru kufanya kazi? Kama watu wanakufa na mtu anasema hakuna ugonjwa mbona hata wakisukumwa hawataenda? Nawaza tu.
Acha awasukume, Yule mama wa elimu kachoka acha. Na bado.

Ugonjwa tujikinge wenyewe haki hamna namna.
 
Huyu naye sasa ni mwongo. Ilikuwa akifika eneo ambalo mtawala ni mpinzani anawaambia wananchi kwamba hawapati maendeleo kwa sababu walichagua mpinzani. Leo tena anakuja na sababu nyingine. Tumweleweje?
Mwishowe atamchapa talaka Mama J kwamba anachelewesha maendeleo!
 
Mimi niliona ni upumbavu kufanyia kazi serikali ya aina hii, nikawatandika 24 hours! Sasa nasikia anatapatapa eti tutafutwe huko tuliko, upumbavu wa kiwango cha lami!
Yani sasa hiyo inakuwa enforcement and no freedom to work
 
Ni ziara ya siku 2, mjini Morogoro, haikuwa mkoa mzima, hakufika Duthumi wala Malinyi wala Kilosa..

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Kala nyama ya mtu....hawezi acha...kawamaliza majirani,Sasa anaanza na watoto wake ....
 
Rais katoa mwelekeo wake kwa kipindi hiki cha miaka mitano ni jukumu la watendaji kufuata maelekezo.

Tanzania ya viwanda inawezekana,

Maendeleo hayana vyama.
Maendeleo hayana vyama?!!! Mbona mlikuwa mnasema wapinzani wanachelewesha maendeleo. Njooni na song jingine, mitano tena
 
Ni mtumishi gani hajafuata maelekezo yake ??

Hakuna mtumishi wa umma anaeweza kukataa maelekezo yake akabaki.

Yeye mwenyewe ndio tatizo kubwa yaani ni zigo haswa.

Ameshaona hana jipya, anatafuta mtu wa kumwangushia jumba bovu Kwasababu anajua hawawezi kumjibu kwasasa.
Inaonekana ameanza kuchanganyikiwa.

Ukifuatilia maneno yake ya hivi karibuni utatambua kuwa sasa amechanganyikiwa hasa.

Mfano mzuri mwingine ni jinsi ya kuikabili COVID-19; sasa anachanganya Mungu, kujifukiza na kidogo kuchanganya mambo ya wananchi kuchukua hatua za kujikinga, lakini kwenye mikutano yake yote hakuna hatua za namna hiyo, kama kuvaa barakoa.

Amekuwa mtu wa kupiga stori tu za jumla jumla bila ya kuwa na msisitizo wowote ili wananchi waelewe nini cha kufanya.

Inamuwia vigumu kufanya hivyo baada ya kujiingiza kwenye kukataa uwepo wa ugonjwa wenyewe na kudharau wanayofanya wengine duniani kote.

Sasa hata akina "comical Ally" wake wanaanza kujichanganya na kukana waliyokuwa wakiyashikia bango, hata kama yalikuwa yanawafanya kuonekana kuwa wajinga.
 
Rais Magufuli amesema kuwa Rais ni kazi ngumu sana kwa sababu wewe unaweza kupanga mipango hii kumbe wenzako nao wana mipango mingine...
Hawa wasaidizi hawawezi badilika,watamkwamisha tu, abadili shria za kodi ziwe rafiki, na kila kitu kiwe digital atakua amepunguza kwa kiasi kikubwa usumbufu na maendeleo yatakuja haraka
 
Ile JF ya wakati fulani huko nyuma huu ungekuwa mjadala wa maana sana na inawezekana ungetafutiwa majibu kuhusu hiyo miradi, hata kama majibu hayo yasingekuwa ya kukuridhisha.

Sasa hivi, unapoteza muda wako, hasa kwa hao uliowa 'cc ' hapo. Nani kati yao hao aliwahi kutoa mchango au mada uliokufanya ukae chini na kuuwaza kwa makini?

Wangalau huyo misuli maana ni kitengo, hao wengine ni Active ndio maana nimewatag.
 
Rais Magufuli amesema kuwa Rais ni kazi ngumu sana kwa sababu wewe unaweza kupanga mipango hii kumbe wenzako nao wana mipango mingine...
Rais hapangi mipango bali inatakiwa ipangwe na Serikali ya Jamhuri ya Muunguno yenye viongozi na watendaji wengi yeye akiwa ni mmoja wao na msimamizi wa shughuli ikiwa ni pamoja na kufuatilia utekelezaji wa Mipango ya Serikali na utendaji wa wale chini yake.

Alifikiri Urais ni rahisi kama kuchunga ng'ombe hata watoto wanatoroka Shule kushinda machingani wakichunga na kucheza. Kuhusu kulalamika hadharani kuwa watendaji wake wanamchelewesha na kutishia kuwa atawafukuza wote toka juu mpaka chini lakini si itabidi ateue wengine mara kwa mara kama alivyofanya Kipindi chote cha kwanza lakini wapya wakaendeleza ucheleweshaji kwa sababu wanafanya Kazi yake kwa maagizo toka kwake na kuyapeleka mbele.

Watendaji wake mara nyingi wanakaa tu wakingoja maagizo ambayo hutolewa kutegemea ameamkaje siku hiyo mara nyingi huja yamechelewa mpaka kusababisha kumchelewesha kwenye mambo yake. Kuomba msaada toka viongozi wa CCM ni kichekesho kingine maana ni Chama hicho ndo kilimleta kwenye mbeleko na kumkabidhi Tanzania yake, Serikali yake, Watanzania wake na Chama chake.

Kusingekuwa na Tanzania ya Magufuli, Serikali ya Magufuli, Wapiga kura wa Magufuli na CCM ya Magufuli angekuwa anawahishwa!
 

Demokrasia bandia na hatari hatari inayolikabili Taifa
 
Rais Magufuli amesema kuwa Rais ni kazi ngumu sana kwa sababu wewe unaweza kupanga mipango hii kumbe wenzako nao wana mipango mingine...

Imekuwaje tena mbona wacheleweahaji walikuwa Chadema na upinzani 😂😂
 
Back
Top Bottom