1000 digits
JF-Expert Member
- Oct 16, 2012
- 7,201
- 9,529
Ni kweli askari wa TZ, Wana kazi kubwa sana ya kuwalinda wananchi hasa watawala lakini mbona maisha yao hamyajari kabisa, kwani ukipita kwenye vibanda vyao wanavyoishi, huwezi amini kabisa! Zamani walikuwa hawalipii umeme kabisa, lakini sasa hivi kila mtu na mita yake! Daaa, na awamu hii waliokuwa wana wasemea japo kidogo huko bungeni ndio, hivyo tena! Wamebakia yatima!! Japo walikuwa wana jiriwaza na pombe za nusu bei kwenye makambi yao, awamu hii hakuna! Ila wanatumikaa!
Maisha ya askari wa Tanzania yanaendana na mazingira ya Mtanzania, wote sisi tunaishi hivyo kama askari wetu pia, ...
Unaona kuwa ni sawa?
Unajua maisha ya wale wanaowatuma?
Maisha ya ma IGP wao ,marpc wao na viongozi wao wengine ambao kiuhalisia wanayoyafanya ni kulinda maslahi yao na si vinginevyo?
Je, mali wanazomiliki viongozi wa serikali na wale wa polisi zinatokana na vipato halali au ndio wale wa kufanya manunuzi hewa na kujichotea mabilioni ya pesa ? Shukrani yao kwa serikali ya CCM inayoendana na matendo yao ya wizi ni kuwadhibiti wapinzani kwa nguvu zote ili uovu wao nao ulindwe?
Kama Serikali ya awamu hii ipo siriasi kupambana na rushwa basi ianze na wale waliopigana kifa na kupona kufanya uhalifu wa kuwapa CCM ushindi wa asilimia 95 + wa ubunge na madiwani.
CCM na viongozi wa Dola wametumia watoto wa maskini walioko kwenye vyombo vya Dola kuwatesa maskini wenzao ili hali wao wanajua wazi kuwa kuwaua watanzania wenzao kwa sababu tu wanagombea uongozi kwa kura ni kosa.
Wanacholinda ni maslahi yao mana Wote ni Watanzania lakini wanachofanyiwa wapinzani utafikiri ni Wasomali wamevamia Tanzania . Kwa nini nguvu kubwa itumike kuwazuia watanzania kupata hata udiwani kwa sababu tu ya vyama? Jibu ni rushwa na maslahi yao yasije yakamulikwa na zimwi lisilokujua