Rais Magufuli yuko vizuri kwenye ulinzi wa mitaji ya umma, yaani public capital kuliko Rais yeyote aliyemtangulia

Rais Magufuli yuko vizuri kwenye ulinzi wa mitaji ya umma, yaani public capital kuliko Rais yeyote aliyemtangulia

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2015
Posts
36,902
Reaction score
52,001
Moja ya majukumu makubwa ya Rais ni kusimamia vizuri mapato na matumizi ya serikali.

Lakini ana kazi ingine kubwa sana ya kusimamia mitaji ya umma ambayo pesa za serikali zimewekwa kwenye vitega uchumi mbalimbali kwenye mashirika ya umma na taasisi ii hiyo mitaji isife.

Tunakumbuka kwa marais waliomtangulia mitaji ya umma mingi ilikufa kwa viwanda kufa, mashirika ya umma kufa na mengine yalikuwa yanapumulia mashine ICU au yanakaribia kufa.

Rais Magufuli kahakikisha mitaji ya umma haikatiki kwa kuyafufua mashirika mengi na kuyajengea uwezo Kama shirika la reli,Air Tanzania no Sasa hivi tunaona yako active Sana.Shirika Kama la bima la taifa lilikuwa linasubiri tu mazishi Sasa hivi liko active sana tu na Lina pesa za uhakika nk.

Asingesimamia mitaji ya umma vizuri mitaji ya umma ambazo ni pesa za kodi za wananchi zilizotumika zisingerudi.

Kumbi nyingi za maofisi na taasisi za serikali zilijengwa kwa mitaji ya umma lakini zilikuwa hazitumiki watu wanakimbilia kumbi za hoteli binafsi wapige pesa na mitaji ya umma ikatike. Sasa hivi zinatumika kikamilifu.

Ukweli Ni kuwa amekuwa akisisitiza watu kutumia huduma ambazo umma umewekeza ili pesa zilizotumika kuanzisha hizo huduma zisipotee na kuhakikisha Kuna usimamizi mzuri sana.

Ndio maana tofauti na kipindi cha waliomtangulia hatuonoi taasisi ya umma ikimfia mikononi mwake hata moja. Akiihisi tu kuwa kuna taasisi yeyote inataka kukata roho anaenda upesi na rescue measure ili kuokoa mitaji ya umma isipotee hapo.
 
Ile miradi ya maendeleo ya Chato kwanini haiwekwi kwenye beti zetu za worship and praise?
 
YEHODAYA,

Hizo ngonjera peleka Lumumba! Mjinga yoyote anaweza kuchota pesa na kupeleka kwenye mashirika ya umma kama ATCL nk kama anavyofanya Jiwe! Lakini hakuna ushahidi wa mashirika hayo kuendeshwa kwa tija!
 
Nimejaribu kutafakari sehemu ambazo Magufuli amezigusa na kuonekana kama Mungu mtu na kubaini kwamba hata 3/10 hajafika na tunaona kinachoendelea, akifanikiwa kusogea na kufika 5/10 Tanzania itakua inchi tishio kwa uchumi Chini ya Jangwa la Sahara. Nitagusa maeneo ambayo JPM hajayagusa kabisa au kayagusa juu juu tu;

1. Wafanya biashara wengi wakati na wadogo hawana leseni za biashara. Ukiachilia mbali maduka ya vyakula na madawa waliobaki wanafanya biashara kiholela sana.

2. Ongezeko la thamani VAT returns ni janga kubwa 2 kati ya biashara kumi ndizo zinatoa risiti baada ya mauzo, ukiachilia mbali Vituo vya mafuta na zile biashara ambazo zinagusika kirahisi na mkono wa sheria.

Mfano; kwa mujibu wa Sheria ya TRA bidhaa yoyote yenye thamani ya sh. 100 inatakiwa kutolewa risiti.

Ni mara ngapi unakunywa sharubati ya miwa pale Ilala na chipsi pale kwa Mdebwedo bila kupewa risiti?

3. Kodi za Nyumba hazilipi ongezeko la thamani VAT wala Kodi ya PATO Mfano mdogo tu! Unakuta nyumba ya vyumba 6 iliyopo Makumbusho kila Chumba mtu anapangishwa kwa Tsh 70,000/- x 6 x 12 unadhani Serikali za mitaa zikiamua kulichukulia hili kama pato lake la maendeleo ya mitaa si mitaa itakua na taa za barabarani?

4. Kusimamia ushuru wa Mazao ya asili na ya kulimwa. Nimeona Wila ya Kisarawe wana geti lao pale kwa ajili ya mazao ya asili (mkaa,miti,mchanga) na geti lao liko very busy tatizo ni kwamba liko kiholela mno na ni rahisi mtumishi kuchukua mapato na kuingia nayo mitini.

5. Faini na Tozo mbalimbali, makosa ya barabarani ya kila siku, mahakamani, vituo vya polisi, faini zetu za mitaani (kumwaga taka, kujisaidia sehemu isiyoruhusiwa, nk)

Mhe JPM kajikita kwenye machache tu ambayo ni Mabenki, Mitandao ya Simu, Madini, watumishi wa umma, safari za Viongozi, semina, mikutano na warsha, rushwa, utalii ameweza kufanya haya yote.

Akigusa na hizo namba tano hapo juu, Tanzania kila raia ataweza kuwa na kadi ya bima ya Afya kwa mwaka kwa shilingi elfu 10 tu.

Wasalaam.
 
YEHODAYA,

Hizo ngonjera peleka Lumumba! Mjinga yoyote anaweza kuchota pesa na kupeleka kwenye mashirika ya umma kama ATCL nk kama anavyofanya Jiwe! Lakini hakuna ushahidi wa mashirika hayo kuendeshwa kwa tija!
Ushahidi upo. mfano kidogo tu Reli ya kwenda Moshi kila ikienda na kurudi Ina abiria kibao Tena daraja la kwanza na la pili

Shirika la bima mafisadi wa maofisini ya serikali walikuwa hawakati bima kule Sasa hivi shirika la bima lina wateja wengi Tena wakubwa halina shida ya pesa. Lilihujumiwa na kampuni za bima binafsi Sasa hivi halionewi Tena

Angalia kumbi za mifisadi serikali hawaendi kwao tena zinajaa za serikali
 
Ile miradi ya maendeleo ya Chato kwanini haiwekwi kwenye beti zetu za worship and praise?
Nimetaja baadhi .Ziko mbuga zilikufa kazifufua Sasa hivi ukienda hata Chato watalii wapo hoteli zinapata wateja biashara zinachangmka watu wanaingiza vipato ambavyo kabla vyanzo hivyo havikuwepo katebngeza vyanzo vipya vya watu wa Chato kupata pesa au wewe ulitakaje vyote vijazwe Kilimanjaro au?
 
Ushahidi upo.mfano kidogo tu Reli ya kwenda Moshi kila ikienda na kurudi Ina abiria kibao Tena daraja la kwanza na la pili

Shirika la bima mafisadi wa maofisini ya serikali walikuwa hawakati bima kule Sasa hivi shirika la bima lina wateja wengi Tena wakubwa halina shida ya pesa .Lilihujumiwa na kampuni za bima binafsi Sasa hivi halionewi Tena

Angalia kumbi za mifisadi serikali hawaendi kwao tena zinajaa za serikali
Biashara ni cashflow, siyo porojo! Hata juzi MV Victoria wamejaza wanaCCM. Mavitu hayo yanaanzishwa ili kupata sifa za kisiasa, hayana mipango endelevu ya kibiashara!
 
Biashara ni cashflow, siyo porojo!
Biashara sio cashflow tu mfano Sasa hivi cashflow ya makampuni ya mafuta Ni kubwa lakini yanatengeneza hasara sababu ya tatizo la Bei soko la dunia!!! Rudi tena darasani kasome upya
 
Na wewe upo kwenye team propaganda? Jiwe amefanikiwa kwenye propaganda kuliko rais mwingine Afrika, na hii ni hatari akimaliza muda wake itakuwa rahisi kupasua baluni.
 
Biashara sio cashflow tu mfano Sasa hivi cashflow ya makampuni ya mafuta Ni kubwa lakini yanatengeneza hasara sababu ya tatizo la Bei soko la dunia!!! Rudi tena darasani kasome upya
Ndiyo maana nakuambia ni rahisi sana kuchota pesa za walipa kodi na kununua mandenge ila kuendesha biashara ya usafiri wa anga ni kitu kingine!

So performance ya mashirika kwa faida ndiyo kigezo cha ufanisi wa kiongozi, tofauti na hapo ni mapambio tu ili watu wapate uteuzi!
 
Sio kweli dunia nzima performance ya ndege za serikali likiwa shirika la umma haipimwi kwa net profit or loss .
Kucheki shirika la umma Kama linafanya vizuri huangalii net profit au loss Kama shirika binafsi

Hili ndio husumbua auditors wengi na financial analyst wengi kuwa how comes shirika la ndege la serikali limepata net loss na serikali inakomaa ku li fund

Serikali inaangalia imeingiza kiasi ganii kupitia Kodi za serikali iambazo mepata eg VAT kupitia tiketi , withholding tax walizolipa watoa huduma kwa shirika nk ukizitoa hizo utashangaa japo shirika la serikali linaonyesha limepata net loss utashangaa serikali inasema linaendeshwa kwa faida.Ila wewe kama ulikariri notes ulikuwa ukisoma Kama robot unasoma ufaulu mitihani haya mambo yako juu ya akili yako net profit serikali inapata dividend Lakini dividend Ni Cha juu tu baada ya serikali kulamba Pesa za VAT per ticket na withholding tax no
Ku analyize shirika la umma kama linapata loss or profit hakuhitaji mwenye low ,IQ Kama wewe hapo Bado Sina analyize other benefits zinazoweza letwa na shirika la umma
 
Kama kuwa na high IQ ni kutetea hasara na uharibifu unaofanywa na Jiwe katika taifa hili ni bora mara elfu kuwa na low IQ!
Kungelikuwa na uhalisia wa unayosema, mahesabu ya ATCL yasingefichwa ikulu!

Kwa namna biashara na uchumi unavyoendeshwa duniani, na approach ya Jiwe, ni dhahiri kuwa legacy yake itakuwa ni ununuzi wa scraps zisizo na faida yoyote!
 
Wewe unaleta hadithi zako za porojo kama vile watu wote wa JF ni wale wajinga wa praise team ya Lumumba.
Kuna mifuko ya jamii ambayo iko chini ya usimamizi wa moja kwa moja na MOF, jee kwa nini imekufa awamu hii hadi kufikia kushindwa kulipa mafao ya kustaafu kwa wenye pesa zao?
Unaelewa waliochangia huko NSSF, PSPF, PPF nk wanateseka kiasi gani kulipwa fedha zao katika awamu hii kuliko ilivyo pata kutokea awamu zilizo pita?
Nyie endeleeni kuchokonoa mambo kumbe mna washtua agenda za kushuka nazo wapinzani wenu kwenye kampeni ya 2020!
Hivi mstaafu ambaye amesota mwaka hajalipwa pesa zake ukimletea story za kufufua ATCL au TTCL ambayo hata hapo Kibamba network haikamati atakuelewa?
Moto mtakutananao, na hapo ujue huyo jiwe wenu atahesabika no mgombea tuu hivyo akileta longolongo jukwaani au fix za push ups anazomewa tuu. Na ule ubabe wa weka ndani yule haupo hapo!
 
Sio kweli dunia nzima performance ya ndege za serikali likiwa shirika la umma haipimwi kwa net profit or loss .
Kucheki shirika la umma Kama linafanya vizuri huangalii net profit au loss Kama shirika binafsi

Hili ndio husumbua auditors wengi na financial analyst wengi kuwa how comes shirika la ndege la serikali limepata net loss na serikali inakomaa ku li fund

Serikali inaangalia imeingiza kiasi ganii kupitia Kodi za serikali iambazo mepata eg VAT kupitia tiketi , withholding tax walizolipa watoa huduma kwa shirika nk ukizitoa hizo utashangaa japo shirika la serikali linaonyesha limepata net loss utashangaa serikali inasema linaendeshwa kwa faida.Ila wewe kama ulikariri notes ulikuwa ukisoma Kama robot unasoma ufaulu mitihani haya mambo yako juu ya akili yako net profit serikali inapata dividend Lakini dividend Ni Cha juu tu baada ya serikali kulamba Pesa za VAT per ticket na withholding tax no
Ku analyize shirika la umma kama linapata loss or profit hakuhitaji mwenye low ,IQ Kama wewe hapo Bado Sina analyize other benefits zinazoweza letwa na shirika la umma
Pammoja na hayo net loss sio abrupt closer ya shughuli za shirika.Yapo mambo mengi ya kuchunguza au kurekebisha na kuboresha.
 
Hongera sana mleta hoja.

Hii ni sehemu ya Hotuba ya Waziri wa Fedha 2020/21
3.2.4.2.1 Benki za Maendeleo
38. Mheshimiwa Spika, benki za maendeleo zinajumuisha Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania - TADB na Benki ya Maendeleo TIB. Kati ya mwezi Julai 2019 na Machi 2020, benki za maendeleo zimetoa mikopo ya jumla ya shilingi bilioni 54.44 sawa na asilimia 32.9 ya kutoa mikopo ya shilingi bilioni 164.84. Kati ya kiasi hicho, Benki ya Kilimo Tanzania ilitoa mikopo yenye thamani ya jumla ya shilingi bilioni 35.86 sawa na ufanisi wa asilimia 176.3 ya lengo la kukopesha shilingi bilioni 20.34 na benki ya TIB shilingi bilioni 18.58 sawa na asilimia 12.86 ya lengo la kukopesha shilingi bilioni 144.5.
Maeneo yaliyopewa kipaumbele ni pamoja na: kilimo, maji, utalii, viwanda vya kuchakata mazao, elimu, makazi, biashara, huduma nyinginezo na madini hususani madini

Mleta hoja kama upo karibu na wakubwa zaidi ya waziri wa Fedha tusaidie kufikisha ujumbe kuwa kuna hela zaidi ya TZS 125.93 bn zimelala TIB na tupo Watanzania wenye nia ya kuwekeza kwenye viwanda ikiwamo kukamua mafuta ya ufuta ambao kwa sasa bei yake imeanguka kwa kutegemea walanguzi toka bara Hindi.

Rejea ushauri kwa mkulu wakati anavunja bunge.
Rais atavunja Bunge la JMT mwezi Juni. Tuko wapi na tunafika lini nchi ya asali na maziwa?

Kama sio urasimu na kuweka vigezo vya kumtaka mwekezaji mzawa atoe 40% ya CAPEX; ni ngumu sana kupata strategic investors kutoka ndani.

Sheria ili mtu awe mbunge ajue kusoma na kuandika ili atunge sheria. Ila akifika bungeni kuna technicals wanamsaidia na kumfunda eventually anaiva. Hata akiingia University graduate hawezi kujua kila kitu, ila anapitia training ndani then anaiva.

Ndivyo ulivyo uwekezaji wa kisasa. Kuna investment consultants kwa kumpa new investor all the tool ikiwamo staff training, management training and system building, marketing management, inventory management, production management whatever you name it; then baada ya muda watu wana- gain skills za kuendesha kiwanda. Tunaingia mwaka mpya wa fedha 87% za fedha zimelala bank, maana yake kuna haja ya kubadili lending system ili kukidhi mahitaji ya uzalishaji sokoni na kurejesha fedha ya mkopo huko kazi zikizalishwa na mazao ya kuchakatwa yakichakatwa.

Mfikishie mzee ili miaka 5 ijayo wale mabilione 1000 wapya nasi tuwemo.

Wasalaam
 
Moja ya majukumu makubwa ya Rais ni kusimamia vizuri mapato na matumizi ya serikali.

Lakini ana kazi ingine kubwa sana ya kusimamia mitaji ya umma ambayo pesa za serikali zimewekwa kwenye vitega uchumi mbalimbali kwenye mashirika ya umma na taasisi ii hiyo mitaji isife.

Tunakumbuka kwa marais waliomtangulia mitaji ya umma mingi ilikufa kwa viwanda kufa, mashirika ya umma kufa na mengine yalikuwa yanapumulia mashine ICU au yanakaribia kufa.

Rais Magufuli kahakikisha mitaji ya umma haikatiki kwa kuyafufua mashirika mengi na kuyajengea uwezo Kama shirika la reli,Air Tanzania no Sasa hivi tunaona yako active Sana.Shirika Kama la bima la taifa lilikuwa linasubiri tu mazishi Sasa hivi liko active sana tu na Lina pesa za uhakika nk.

Asingesimamia mitaji ya umma vizuri mitaji ya umma ambazo ni pesa za kodi za wananchi zilizotumika zisingerudi.

Kumbi nyingi za maofisi na taasisi za serikali zilijengwa kwa mitaji ya umma lakini zilikuwa hazitumiki watu wanakimbilia kumbi za hoteli binafsi wapige pesa na mitaji ya umma ikatike. Sasa hivi zinatumika kikamilifu.

Ukweli Ni kuwa amekuwa akisisitiza watu kutumia huduma ambazo umma umewekeza ili pesa zilizotumika kuanzisha hizo huduma zisipotee na kuhakikisha Kuna usimamizi mzuri sana.

Ndio maana tofauti na kipindi cha waliomtangulia hatuonoi taasisi ya umma ikimfia mikononi mwake hata moja. Akiihisi tu kuwa kuna taasisi yeyote inataka kukata roho anaenda upesi na rescue measure ili kuokoa mitaji ya umma isipotee hapo.
Air Tanzania ilikufa ikiwa na ndege 13 wakati yeye akiwa Waziri wa Uchukuzi kwa hiyo lilikufa kwababu ya uongozi wake mbaya. Kujaribu kurekabisha udhaifu wake akaanzisha upya Shirika hilo lakini likafa kabla hata halijaanza huku , madege na mabawa yao yakiwa yamepark uwanjani. Usafiri wa Treni Dar-Tanga-Moshi-Arusha ulisita wakati akiwa Waziri wa Uchukuzi. Sasa toka ameingia madarakani amekuwa anajaribu kuanzisha tena lakini watu Mikoa ya Kaskazini bado wanasubiri usafiri wao wa miaka zaidi 100 uanze tena. Mambo mengi yaliharibika akiwa Waziri ikiwa ni pamoja na Ferry ya Bagamoyo, samaki wake na mengine mengi. Wengi tunashangaa pamoja na madudu hayo yote aliwezaje kukaa kwenye Uwaziri miaka 20 chini ya Marais wawili? CCM lolote linawezekana!
 
Back
Top Bottom