Kiingereza ni muhimu katika dunia ya leo lakini isionekane ndo big agenda kila siku huyu hajui kiingereza hajui kiingereza as if Rais akijua kiingereza ndo basi tena!!
Tukirudi kwa Mkapa, background inambeba zaidi Mkapa ukimlinganisha na JPM au hata JK! Tusisahau, Mkapa ali-graduate Makerere degree in English. Sasa unaweza kupata picha kwa umri wa Mkapa miaka hiyo pale Makerere kulikuwa na walimu wa aina gani. Ukichanganya na ukweli mmwingine kwamba hata Masters yake alisomea kwenye English speaking country na kuhudumu Foreign affairs kwa takribani miaka 10; bado yote hayo yana nafasi kubwa sana ya kumfanya BM awe mzuri kwenye Kikoloni... ambacho angehitaji cha ziada ni confidence kitu ambacho pia anayo!
Sasa huyu mwenzetu ambae hamuishi kumsemanga; kwanza kazaliwa sehemu ambayo hadi leo hata Kiswahili bado shida! From Standard I to PhD kasomea kwenye local institutions. Making things worse, masomo aliyosoma hayahitaji competency in English! Kuingia kwenye ajira, from ajira yake ya kwanza, hadi ya mwisho kabla ya urais ni zile ambazo tunaweza kusema local posts! Manake bora ingekuwa ameshawahi kuhudumu hata Waziri wa Fedha tungesema alishapata uzoefu wa kukaa kwenye negotion tables mbalimbali za watumia kikoloni! Lakini mara leo waziri wa mifugo... hapa labda alihitaji kukifahamu Kimasai zaid kuliko hicho Kiingereza... mara kesho wa waziri wa Ujenzi... wadau wake ni Wachina ambao hata hicho Kiingereza chenyewe hawakijui!! JK nadhani ile miaka 10 ya foreign affairs ilim-shape sana!!