Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Inaelezwa kuwa huu ni moja ya wimbo mkubwa zaidi wa kueneza propaganda iliyowahi kutengenezwa Afrika na Duniani kwa ujumla. Wimbo huu uliimbwa na Mwanamuziki Nguli wa Muziki wa Rhumba kutoka nchini Zaire(DR Congo kwa sasa), Franco Luambo Luanzo Makiadi mnamo 1984 wakati wa vuguvugu la uchaguzi wa Urais wa Zaire.
Mobutu alikuwa ndiye mgombea pekee na uchaguzi huo ulikua na aina mbili tu ya kura ya "ndio" au "hapana". Kulingana na matokeo rasmi, 99% walipiga Ndio kwa Mobutu.
Ingawa Mobutu alikuwa ndiye mgombea pekee, laikini inaelezwa kuwa alipiga kampeni kali nchini kote akipeleka ujumbe wake katika ukingo wa kwanza wa nchi na wa mwisho. Na wimbo huu ulikuwa nguzo yake muhimu ya propaganda.
Wmbo huu una takribani dakika 19 hata albamu ya wimbo huu ilipotolewa, wimbo ulirudiwa kwa pande zote A na Upande B.
Ulisambazwa bure kwa Wazaire wote. Kava ya albamu haikuwa na jina la Franco lakini wimbo ulipewa sifa.