M24 Headquarters-Kigali
JF-Expert Member
- Jul 9, 2012
- 8,199
- 8,186
Mkuu AFCON yenyewe ni ndoto tena ya mchana kweupeee! Sasa sijui tutawezaje kuingia na kutwaa World cup wakati tumewahi kuvuzu michuano ya Africa maramoja tuu tangu tupate Uhuru.Nchi hii tulibahatika kupata rais mpenda michezo kwa miaka kadhaa, tunaomba awamu hii ihakikishe Taifa Stars inaingia na kutwaa WORLD CUP 2018
Siku tukiweza kuwafunga Waarabu tu ndipo kila kitu kitawezekana maana Timu za misri zinaionea Tanzania kuanzia vilabu mpaka Timu ya Taifa , hata Yanga Safari imeiva tayari kule wakienda hawachomoki hata wangekuwa wamemsajili Mess na Ronaldo pale Mbele.Vipi Tanzania hatuendi Rio 2016!!!
Tanzania mpira unachezwa nje ya uwanja Kwa waganga wa kienyeji na Rushwa kununua mechi kumewafanya wachezaji kubweteka matokeo yake kwenye mechi za kimataifa wanaumbuka maana kunakuwa hakuna njia ya kamati za Ufundi kusaka matokeo nje ya uwanja.Wizara, vyama vya michezo na klabu za Tanzania wamejaa wababaishaji wasiojua thamani ya michezo. Hebu tizama nchi kama Kenya & Ethiopia wanavyotuzidi kwenye Riadha sisi labda tukacheze BAO, KARATA & POOL TABLE.
Mkuu huko kote mbali Kama tumeshindwa kuwafunga Waarabu ambao Timu zingine zinawafunga unadhani Soka litakua ? Tanzania bado ni kichwa cha mwendawazimu kwenye michezo mpaka siku Magufuli akiamua Kuunda Wizara pekee ya Michezo isiyochanganywa na mambo mengine na apewe Waziri na naibu Waziri na katibu mkuu wapenda michezo na watu makini na wakereketwa wa maendeleo ya michezo , kinyume na hapo michezo itaendelea kudumaa zaidi kwenye awamu hii ya Magufuli .Mkuu AFCON yenyewe ni ndoto tena ya mchana kweupeee! Sasa sijui tutawezaje kuingia na kutwaa World cup wakati yumewahi kuvuzu michuano ya Africa maramoja tuu tangu tupate Uhuru.
Ndoto ni nzuri lakini ni bora tuote kinachoendana na hali halisi, me nashauri tuwekeze zaidi kwenye ligi za chini, ligi kuu VPL, michuano ya Kagame, CHAN, AFCON ndio World cup.
Ushauri mwingine michezo sio mpira wa miguu tuu, kuna michezo mingi sana ambayo inaweza kuajiri vijana na kuliletea taifa sifa kubwa. Kama tumeshindwa mpira wa miguu tujaribu michezo mingine kama tennis, golf,basketball, riadha,kuogelea,rugby,cricket, nk.......
hivi ni tangu tumepata uhuru au tangu michuano hiyo ianzishwe?Mkuu AFCON yenyewe ni ndoto tena ya mchana kweupeee! Sasa sijui tutawezaje kuingia na kutwaa World cup wakati yumewahi kuvuzu michuano ya Africa maramoja tuu tangu tupate Uhuru.
Ndoto ni nzuri lakini ni bora tuote kinachoendana na hali halisi, me nashauri tuwekeze zaidi kwenye ligi za chini, ligi kuu VPL, michuano ya Kagame, CHAN, AFCON ndio World cup.
Ushauri mwingine michezo sio mpira wa miguu tuu, kuna michezo mingi sana ambayo inaweza kuajiri vijana na kuliletea taifa sifa kubwa. Kama tumeshindwa mpira wa miguu tujaribu michezo mingine kama tennis, golf,basketball, riadha,kuogelea,rugby,cricket, nk.......
Mkuu ni tangu michuano ianzishwe. Ila si unajua kipindi kabla ya Uhuru tulikuwa chini ya mkoloni, kwahiyo maslahi ya kiuchumi kwa mkoloni yaliwekwa mbele kuliko masuala ya michezo, AFCON ilianzishwa. mwaka 1957, FIFA world cup 1930.hivi ni tangu tumepata uhuru au tangu michuano hiyo ianzishwe?