Rais mpya mwanamke wa Namibia kateua Makamu mwanamke na mawaziri 8 kati ya 14 wote ni wanawake

Rais mpya mwanamke wa Namibia kateua Makamu mwanamke na mawaziri 8 kati ya 14 wote ni wanawake

MTV MBONGO

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2016
Posts
1,288
Reaction score
1,262
Rais mpya wa Namibia, Netumbo Nandi-Ndaitwah, ametangaza Baraza lake la Mawaziri kwa mara ya kwanza siku ya Jumamosi, akimteua Lucia Witbooi kuwa makamu wa rais wa kwanza mwanamke katika historia ya nchi hiyo.

Namibia sasa ni nchi pekee barani Afrika yenye rais na makamu wa rais wote wanawake.

Nandi-Ndaitwah ameapisha mawaziri 14, ambapo wanane kati yao ni wanawake, pamoja na manaibu saba katika mji mkuu, Windhoek.

"Sina shaka kwamba tutatekeleza majukumu ambayo watu wa Namibia wametupa," alisema.

Aliongeza kuwa wizara za serikali zinapaswa kuweka mipango ya kutokomeza umasikini.

"Masuala ya makundi yaliyotengwa na wenye ulemavu yatawekwa chini ya ofisi ya makamu wa rais ili kupata uangalizi wanaohitaji," alisema, huku akiwaomba wananchi wa Namibia kuwapa nafasi mawaziri wake kutekeleza majukumu yao.

Uteuzi mwingine muhimu ni Elijah Ngurare kama waziri mkuu na Selma Ashipala-Musavyi kama waziri wa mahusiano ya kimataifa na biashara.

Source: AA
 
Hai wapumbavu wameshindwa hata kula chabo kwa jirani??
Wamefeli tayari, mapungufu ya huko nyuma yanaenda kuwacost kwenye ripoti ya CAG labda wawe mafundi wa kufunga bao la mkono kama dada yangu
 
Hai wapumbavu wameshindwa hata kula chabo kwa jirani??
Wamefeli tayari, mapungufu ya huko nyuma yanaenda kuwacost kwenye ripoti ya CAG labda wawe mafundi wa kufunga bao la mkono kama dada yangu
Wanawake wakiwezeshwa, wanaweza
 
Hai wapumbavu wameshindwa hata kula chabo kwa jirani??
Wamefeli tayari, mapungufu ya huko nyuma yanaenda kuwacost kwenye ripoti ya CAG labda wawe mafundi wa kufunga bao la mkono kama dada yangu
Kule Malawi alishika urais akataka kuingiza nchi kwenye vita ambavyo isingeshinda,wanaume walikaa mezani wakatuliza Hali,huku kwetu Kuna matumizi yasiyo yalazima billioni 37++,ngoja huko mbele watalia tu
 
Kwanini Wananchi wa Taifa la Namibia,wasitembelee Tanzania,waone huyu mama anakotuteleka hadi tunajuta
 
Back
Top Bottom