Rais mpya wa Namibia, Netumbo Nandi-Ndaitwah aliishi kwa miaka 6 Dar es Salaam miaka ya 1980’s. Mwalimu Nyerere alikuwa akimuita “Mama wa SWAPO”

The Sheriff

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2019
Posts
747
Reaction score
2,112
Namibia.png

Rais wa kwanza mwanamke Namibia, Netumbo Nandi-Ndaitwah

Namibia imepata Rais wa kwanza mwanamke, hatua kubwa katika historia ya taifa hilo. Safari yake ya kuwa mwanamke wa kwanza katika mambo ya kisiasa haijaanzia hapo alipo. Mwaka 2017 alichaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa SWAPO, akiwa mwanamke wa kwanza kushika nafasi hiyo.

Lakini pia Netumbo Nandi-Ndaitwah amekuwa mgombea wa kwanza mwanamke wa urais kupitia chama cha SWAPO katika uchaguzi mkuu wa Namibia wa mwaka 2024.

Kihistoria, mama huyu amehudumu kwa miongo mingi ndani ya chama chake, tangu enzi za kupigania uhuru. Na kuanzia mwaka 1980 hadi 1986, Netumbo Nandi-Ndaitwah alikuwa Mwakilishi Mkuu wa SWAPO kwa Afrika Mashariki, akiwa na makao yake jijini Dar es Salaam. Jambo hili amewahi kuliongelea akiwa Tanzania, ambapo alinukuliwa akisema:

“Natumai, kama mimi, nyote mnajisikia kuwa nyumbani licha ya kuwa mbali na nyumbani. Kwangu mimi, baada ya kuhudumu katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama Mwakilishi wa SWAPO katika miaka ya 80, Dar es Salaam ni kweli nyumbani, na inanirudisha kwenye kumbukumbu za Mwalimu Nyerere, mzalendo wa kweli wa Afrika. Kwangu, Mwalimu alinifahamu tu kama Mama wa SWAPO.”

Mhe. Netumbo aliyasema maneno hayo katika taarifa yake ya kuaga kama mwenyekiti anayemaliza muda wake wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), akiwa pia Naibu Waziri Mkuu wa Namibia. Ilikuwa ni katika Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC uliofanyika tarehe 13 Agosti 2019 jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Ikumbukwe tu kwamba kuibuka kwa harakati za ukombozi barani Afrika baada ya Vita vya Pili ya Dunia lilikuwa jambo muhimu katika kufanikisha uhuru wa mataifa mengi ya Afrika. Tanzania, chini ya Hayati Mwalimu Julius Nyerere, ilifanya kazi kubwa na muhimu katika kusaidia harakati hizo, na ilikuwa mpinzani thabiti wa ukoloni barani Afrika.

Tanzania ilijitolea kama kituo cha msaada kwa wale waliokuwa wakipigania ukombozi. Tanzania ilihifadhi vikosi vya harakati nyingi za ukombozi, zikiwemo: African National Congress (ANC) na Pan African Congress (PAC) kutoka Afrika Kusini, Mozambique Liberation Front (FRELIMO) kutoka Msumbiji, People’s Movement for the Liberation of Angola (MPLA) kutoka Angola, Zimbabwe African National Union (ZANU) na Zimbabwe African People’s Union (ZAPU) kutoka Zimbabwe, pamoja na South West Africa People’s Organisation (SWAPO) kutoka Namibia.
 
Hawa wote kina Eduardo Mondlane (Msumbiji), Robert Mugabe (Zimbabwe) Kanyama Chiume (Malawi), Frederick Chiluba (Zambia), Joseph Kabila (DRC), Yoweri Museveni (Uganda), John Garang (Sudan ya Kusini), Thabo Mbeki (Afrika ya Kusini) wameishi Tanzania.
 
View attachment 3168539
Rais wa kwanza mwanamke Namibia, Netumbo Nandi-Ndaitwah

Namibia imepata Rais wa kwanza mwanamke, hatua kubwa katika historia ya taifa hilo. Safari yake ya kuwa mwanamke wa kwanza katika mambo ya kisiasa haijaanzia hapo alipo. Mwaka 2017 alichaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa SWAPO, akiwa mwanamke wa kwanza kushika nafasi hiyo.

Lakini pia Netumbo Nandi-Ndaitwah amekuwa mgombea wa kwanza mwanamke wa urais kupitia chama cha SWAPO katika uchaguzi mkuu wa Namibia wa mwaka 2024.

Kihistoria, mama huyu amehudumu kwa miongo mingi ndani ya chama chake, tangu enzi za kupigania uhuru. Na kuanzia mwaka 1980 hadi 1986, Netumbo Nandi-Ndaitwah alikuwa Mwakilishi Mkuu wa SWAPO kwa Afrika Mashariki, akiwa na makao yake jijini Dar es Salaam. Jambo hili amewahi kuliongelea akiwa Tanzania, ambapo alinukuliwa akisema:

“Natumai, kama mimi, nyote mnajisikia kuwa nyumbani licha ya kuwa mbali na nyumbani. Kwangu mimi, baada ya kuhudumu katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama Mwakilishi wa SWAPO katika miaka ya 80, Dar es Salaam ni kweli nyumbani, na inanirudisha kwenye kumbukumbu za Mwalimu Nyerere, mzalendo wa kweli wa Afrika. Kwangu, Mwalimu alinifahamu tu kama Mama wa SWAPO.”

Mhe. Netumbo aliyasema maneno hayo katika taarifa yake ya kuaga kama mwenyekiti anayemaliza muda wake wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), akiwa pia Naibu Waziri Mkuu wa Namibia. Ilikuwa ni katika Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC uliofanyika tarehe 13 Agosti 2019 jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Ikumbukwe tu kwamba kuibuka kwa harakati za ukombozi barani Afrika baada ya Vita vya Pili ya Dunia lilikuwa jambo muhimu katika kufanikisha uhuru wa mataifa mengi ya Afrika. Tanzania, chini ya Hayati Mwalimu Julius Nyerere, ilifanya kazi kubwa na muhimu katika kusaidia harakati hizo, na ilikuwa mpinzani thabiti wa ukoloni barani Afrika.

Tanzania ilijitolea kama kituo cha msaada kwa wale waliokuwa wakipigania ukombozi. Tanzania ilihifadhi vikosi vya harakati nyingi za ukombozi, zikiwemo: African National Congress (ANC) na Pan African Congress (PAC) kutoka Afrika Kusini, Mozambique Liberation Front (FRELIMO) kutoka Msumbiji, People’s Movement for the Liberation of Angola (MPLA) kutoka Angola, Zimbabwe African National Union (ZANU) na Zimbabwe African People’s Union (ZAPU) kutoka Zimbabwe, pamoja na South West Africa People’s Organisation (SWAPO) kutoka Namibia.
Huyo mbibi anaenda ikulu kufanya Nini 🏃 🏃 🏃 🏃
 
Back
Top Bottom