Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akutana na Rais wa Nigeria

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akutana na Rais wa Nigeria

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
3,978
Reaction score
6,739
Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, kwa nafasi yake ya Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Ubia wa Elimu Duniani (GPE) amekutana na Rais wa Nigeria kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Taasisi hiyo na Nigeria.

Rais mstaafu Kikwete amemweleza nia ya Taasisi hiyo kutaka kuiomba Nigeria kuwa mwenyeji mwenza wa kampeni ya kuchangia fedha za kufadhili miradi ya GPE kwa kipindi cha mwaka 2021-2025 sambamba na nchi ya Ufaransa.
Screenshot_20250129_181131_Lite.jpg


Taasisi ya GPE iliyoanzishwa na nchi zenye uchumi mkubwa duniani (G7), imejiwekea utaratibu wa viongozi wawili, mmoja kutoka nchi iliyoendelea na mwingine kutoka nchi inayoendelea kushirikiana katika kuongoza kampeni ya kuhamaisha nchi zilizoendelea na zinazoendelea kuchangia fedha za kuendesha miradi ya Taasisi hiyo inayolenga kusaidia jitihada za nchi mbalimbali kutimiza lengo la 4 la Maendeleo endelevu la kumpatia kila mtoto elimu bora, na yenye usawa na kutoa fursa kwa wote kujiendeleza.

GPE imejikita kutekeleza miradi yake katika nchi masikini zaidi na zinazokabiliwa na changamoto kama vile vita, athari za mabadiliko ya tabianchi, nk. Viongozi wanaomaliza muda wao katika nafasi hiyo ni waliokuwa Waziri Mkuu wa Uingereza, Borris Johnson na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya.
 
Back
Top Bottom