Rais mstaafu, Jakaya Mrisho Kikwete atakumbukwa milele kwa kuimarisha demokrasia nchini

Rais mstaafu, Jakaya Mrisho Kikwete atakumbukwa milele kwa kuimarisha demokrasia nchini

Mwizukulu mgikuru

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2021
Posts
5,715
Reaction score
13,739
Rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete ni kiongozi miongoni mwa viongozi pekee barani Afrika walioweza kuimarisha demokrasia nchini japo kuna baadhi ya madhaifu machache yaliyoweza kuripotiwa, mfano utekwaji wa mwenyekiti wa madaktari Dk. Ulimboka, lakini tukiondoa madhaifu haya Rais mstaafu Dkt, Jakaya Mrisho Kikwete atabaki kuwa ndie Rais bora zaidi toka uhuru, alieweza kuimarisha demokrasia nchini kwa kuwapa upinzani uhuru wa kujieleza na mengineyo..
 
Mbali na ufisadi kukomaa sana wakati wake na kusafiri safiri mno mpaka akabatizwa Uvasco Da Gama na wanaCHADEMA huku akiitwa kiongozi dhaifu na goigoi (japo akina Ulimboka na Mwangosi wanaweza kuwa na maoni tofauti), Kikwete angeacha legacy moja kubwa sana sema alifeli katika mambo makubwa mawili:

1. Alitia sahihi sheria ya makosa ya mtandao - sheria mbovu ambayo ililalamikiwa sana na kila mpenda uhuru wa habari. Sheria hii ilikwenda kinyume na mengi aliyoyahubiri kuhusu uhuru wa habari na demokrasia. Hili lilikuwa ni kosa katika legacy yake ya kukuza demokrasia!

2. Alishindwa nini kutupatia katiba ile mpya ya Warioba? Mchakato aliuanzisha yeye. Nchi nzima kamati ikazunguka kukusanya maoni. Ikatumia mabilioni ya shilingi. Katiba mpya nzuri ikapatikana. Bunge la katiba likakaa. Likatafuna mabilioni ya shilingi. Halafu akaenda bungeni na kuikana katiba ile - katiba ambayo ingetuondolea matatizo yetu mengi tu. Hili jambo huwa linanisikitisha sana maana alipoteza legacy nzuri ya kuingia katika historia kama rais ambaye alituletea mageuzi ya kweli; na kuiweka nchi katika mwelekeo mpya.

Kila nikimkumbuka JK huwa nasikitishwa sana na haya mambo mawili - hasa hili la pili. Viongozi wakuu na wenye kuacha alama za kudumu huwa na sifa ya kuchukua maamuzi magumu hata kama yanakwenda kinyume na falsafa na maslahi ya vyama vyao kwa faida ya vizazi vijavyo. Na Kikwete hakuwa kiongozi wa aina hiyo.

Vinginevyo mtacheka naye sana tu lakini kuwa mwangalifu...ila angalau alituletea mbaya wako Magufuli; japo yalipomshinda alisarenda (if you know what I mean!). Na watu wazuri hawafi!🚶🏿‍♂️🚶🏿‍♂️🚶🏿‍♂️🚶🏿‍♂️🚶🏿‍♂️
 
Rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete ni kiongozi miongoni mwa viongozi pekee barani Afrika walioweza kuimarisha demokrasia nchini japo kuna baadhi ya madhaifu machache yaliyoweza kuripotiwa, mfano utekwaji wa mwenyekiti wa madaktari Dk. Ulimboka, lakini tukiondoa madhaifu haya Rais mstaafu Dkt, Jakaya Mrisho Kikwete atabaki kuwa ndie Rais bora zaidi toka uhuru, alieweza kuimarisha demokrasia nchini kwa kuwapa upinzani uhuru wa kujieleza na mengineyo..
Kumzidi Samia? Huyo huyo aliyeshindwa kuzuia mauaji ya Mwanndishi wa Habari Iringa na Wafuasi wa Machadema eg Mawazo?

Huyo huyo aliyekuwa anagombana na waandamanaji Kila kukicha?

Kipi anachiweza mzidi Samia kwenye Demokrasia Kwa mfano?
 
Back
Top Bottom