Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete kuhudhuria harusi ya Alikiba jijini Nairobi Kenya

Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete kuhudhuria harusi ya Alikiba jijini Nairobi Kenya

Diamondi asiache kwenda kula pilau ya rafiki yake
 
vya ndani ndio akina Nandy, Sancho na Sepetu
acha kabisa ..ukiwa mmoja wapo hapo utachekwa mpaka na kuku" hata" shetani nae atafuta urafiki nawe ""maana ataona daahh huyu rafiki yangu sasa amevuka mipaka"" ameamua kuyaleta matatizo nyumbani kwake yeye Mwenyewe!!!
 
Ndoa ya mwanamuziki Alikiba na mchumba wake Amina inatarajiwa kufungwa kesho alfajiri katika msikiti wa Ummul Kulthum ulioko eneo la Kizingo jijini Mombasa.


Mama wa bibi harusi mtarajiwa, Bi Asma Said anasema ndoa hiyo itafungwa katika msikiti huo uliojengwa na Gavana wa Mombasa, Hassan Joho.
Anasema baada ya ndoa kufungwa itafuatiwa na sherehe ya kupambwa bibi harusi ambayo itafanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini humo.


Miongoni mwa watu mashuhuri wanaotarajiwa kuhudhuria harusi hiyo ni Rais wa Awamu ya nne, Jakaya Kikwete na Ommy Dimpoz.



Akizungumza na Mwananchi Bi Asma anasema maandalizi yanaendelea vizuri na nyumbani
kwa bibi harusi mwandishi alishuhudia wanawake wakiwa wanajipamba huku wengine wakijipaka henna.



Alibainisha kuwa tayari bwana harusi ameingia nchini Kenya huku wadokezi wakisema kuwa Alikiba alikuwa katika hoteli ya English Point Marina ambapo ni karibu na nyumba ya bibi harusi iliopo eneo la Kongowea.



“Kijana ametoka Tanzania na kuja kuoa Kenya mimi sikujua kama mtoto wangu ataolewa na Alikiba lakini Mungu ndio aliyepanga,” akasema Bi Asma.
Unaandika Nairobi na ndani unaelezea Mombasa hujui hata hilo dogo kwamba Mombasa si Nairobi
 
Back
Top Bottom