Rais Mstaafu Kikwete aliwahi kulalamika kutengwa na majirani zetu, siyo wa kuwaamini sana

Tuwe na staha bandugu
Tz ni yetu sote ushauri ni jambo jema kwa faida ya Taifa
Majirani zetu sio wa kuwaamini kiviiilee
Mama ashauriwe vyema taratibu na hawa watu
Huku kukurupuka 'italigharimu Taifa'
Kenya watakuja kununua mbao korosho kahawa mahindi Maparachichi kwa bei ndogo wakauze nje waseme ni mali ya Kenya

Serikali iwaamuru waje wajenge viwanda ndani ya Tanzania na kutumia airport na Bandari zetu kuimport na export.
Mahindi yasafirishwe kupitia bandari ya Dar kwenda Mombasa kuua panya road
Maparachichi wajenge viwanda kunakozalisha zao hili na kusafirisha nje

Vyote iwe ni Mali ya Tz sio Kenya
Hapo tutakwenda sawa si vinginevyo
 
Kwani uhuru ameomba kitu toka kwetu? Uhuru hajawahi kanyaga Chatto mzee ni Raila
Ni kweli siasa ikiingia kwenye ubongo, ubongo unakuwa hauna kazi tena?
Yaani kabisa unabisha Kenyatta hajawahi kwe da chato? Kenyatta na Magufuli walikuwa marafiki, achana na hiyo misuguano ya kimaslahi uliyokuwa unaiona.
Haya habari hii hapa, ukitaka naa video niambie maana alilala kabisa huko chato asubuhi akapewa tausi akasepa
 
mkuu unachokisema ni sawa lakini a story has always 2 sides you have jst narated one side of the story,kwaiyo ni swala la kuketi na kuweka mambo sawa bila uzito kuegemea pande moja.
 
Tukumbuke pia kuvunjika kwa Jumuia ya Afrika, 1977, hadi Rubani wa Tz kutorosha ndege moja na Shirika la Reli kugawanyika.

Mwaka 1977, Jumuiya ya Afrika Mashariki ilivunjika kutokana na Kenya kuomba viti zaidi katika vyombo vya kufanya maamuzi, kutoelewana kati ya nchi wanachama, na mifumo tofauti ya kiuchumi kati ya nchi, hasa kati ya Tanzania na Kenya.

Hivyo, Serikali ya Awamu ya Sita isipokuwa makini, kujitegemea tulikoanza kuonja tutarudi kule kule kuwa tegemezi wa bidhaa za viwanda vya Kenya na tukabaki kuwauzia malighafi. Iwapo viwanda vyetu vitasimama kwa sababu ya ushindani, ndoto za ajira 8m zitabaki kuwa ndoto.
 
Photoshop mkuu
 
Hata hiyo gesi ni mauzauza kwn tulishaambiwa gesi ni ya mabeberu..labda kama mnazungumzia gesi tofauti
 
Nimeona niliweke sawa maana ilionekama Kama Magufuli alikuwa mkorofi kumbe hata Kikwete walikuwa hawaelewani nae
Tumia akili na ujiuljze mbona hizo nchi tatu ziliamua zije pamoja wafanye kazi kwa umoja.

Fikiria hayo na ujijazie
 
mkuu unachokisema ni sawa lakini a story has always 2 sides you have jst narated one side of the story,kwaiyo ni swala la kuketi na kuweka mambo sawa bila uzito kuegemea pande moja.
Kabisa, wao wameskia side moja wakaidandia kama dala dala. Na pia mbona hamjiulizi kwa nini hizi nchi tatu ziliamua kufanya kazi pamoja na kuitenga 🇹🇿.

Kufikiria ni bure lakini duuh
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…