Rais Mteule Barack H. Obama!

The White House is now being painted Black. Open and see the photos in the attachement below!!!!!!!!!!!!!

Naomba mtu anisaidie kuibadika hapa, mimi huo utaaramu sina.
 

Attachments

Unajifanya umesahau siyo?

"There is a new Sheriff in town"

Nimesahau nini? au unazungumzia wager yako na LeanBack?

Tuma hizo specs na mimi nitazifikisha kwake.....kichaa wangu huyo
 

Nataka nikuulize maswali wewe Muheshimiwa? BHO kwa kupata malezi ya mama/bibi yake mzungu na baba mu-indonesia amegeuka kuwa MZUNGU? Nataka nikuulize swali lingine. Hivi wanaotelekeza watoto ni watu weusi tu ikiwa na maana wazungu huwa hawatelekezi watoto?

Muheshimiwa kama BHO alitelekezwa na Baba yake sisi hayatuhusu! Hayo ni maisha yake binafsi na binafsi sijawahi kusikia AKILALAMA hadharani. Yanayotuhusu ni Historia aliyoaiandika huyu KIJANA! Kumbuka tukio hili limetokea baada ya miaka mingapi ya utabiri wa MLK!

BHO awe alitelekezwa au hakutelekezwa anabakia kuwa ni Mmarekani Mweusi Tii wa kwanza kuingia Jumba Jeupe hivyo basi na sisi binamu zake Waafrika Weusi Tii tunashangilia kuanzia huko huko kwa kina P Diddy, Senti Hamsini hadi huku Kegelo kwa kina Jaramogi na hata kule kusini kwa kina Zuma na kule Ufaransa kwa kina 'cheusi' Thuram hadi kule kwa kina Ze Mariaz LEO ni RAHA TUPU! Hayo ya kutelekezwa mfufue BHO Snr labda atakuomba radhi kwa niaba ya 'wazungu' wenzio (Bwa ha ha haaaa!) na atakuelewa na atakwenda kumuomba radhi BHO jnr! Vinginevyo kwa raha zetu tuache tusherehekee. Hapa nilipo kifuani kwangu nina Beji ina picha ya Obama ikiwa imeandikwa 'Obama'08 for President!' Nakatiza mitaa ya Kibena, Njombe! Hurrraaayyyyy!
 
Nipo....kwa nini nikimbie? Maisha yanaendelea na tutapata fursa ingine 2012 na Bobby Jindal.....

Teh Teh teh teh

ha hahaha hahaha
Nimefurahi sana kukuona NG, nilipatwa naofu kwa kuwa sijakuona leo.

Bora umefika maana kidogo watu walitaka kuanza kutangaza kuwa Umechanganyikiwa kwa kushindwa hadi umepotea njia, eti uliingia nyumba ya jirani, ya kweli hayo?

Tupo Pamoja Mkuu!
 

Give the best to your children, you never know what they gonna be!

Nimejifunza mengi toka kwa Obama from hard work, to caring. I like the way he treats his family (mkewe na watoto). The pursuit of success.
 
Bora umefika maana kidogo watu walitaka kuanza kutangaza kuwa Umechanganyikiwa kwa kushindwa hadi umepotea njia, eti uliingia nyumba ya jirani, ya kweli hayo?

Poor investor Nyani Ngabu aka McCain aka Leanback .......unatoa ndizi Mwanza na kupeleka Bukoba.
 

KITU KIKUBWA AMBACHO KIMENIFURAHISHA KWENYE HUU UCHAGUZI WA MAREKANI NI CONCESSION SPEECH YA MGOMBEA WA REPUBLICAN NDUGU MACCAIN. YAANI NIMEJISIKIA NYWELE ZINASISIMKA. KWELI TUFANYE TUFANYALO, ILA DEMOKRASIA YA MAREKANI IMEKOMAA SANA.

HATA UKIANGALIA VITI VYA SENATE AU HOUSE OF REPRESENTATIVE. MTU ANASHINDWA KWA MARGIN NDOGO SANA, LAKINI ANACONCEDE PALE PALE.

IAM NOT AN AMERICAN BUT I AM OVERWHELMINGLY IMPRESSED BY THE WAY THEY HOLD DEAR THEIR DEMOCRACY. IMAGINE THE WHOLE WORLD WAS WATCHING. PERHAPS ITS BECAUSE MOST OF US WE CANT SEE THE SAME HAPPENING IN OUR COUNTRIES.

THATS MY CONVICTION, ANY COUNTRY WHICH HOLD DEAR ITS DEMOCRACY AND RIGHTS OF ITS CITIZENS, WILL MOST LIKELY ENDURE AND PROVE WRONG ITS CRITICS. (contrast na Russia ambayo leo rais wake ameliambia bunge waongeze muhula wa kutawala uwe miaka sita baadala ya minne! Africa is a sad case..we cant compare...)

GO BLESS AMERICA, GOD BLESS AFRICA!
 

Watu weupe nao wanatelekeza wanao. Mfano ni baba yake Robert Nesta Marley. Kwa bahati mbaya tunaoongoza kwa kutelekeza watoto ni sisi weusi. Nyumba nyingi huko Marekani katika jamii ya watu weusi zinaongozwa na wanawake maana wakina baba ama wako MIA au wako jela!

Barack Obama ni mweusi kwa vile yuko marekani ambako kuna kitu kinaitwa One drop rule. Angekuwa kwetu tungemsimanga kwa kumuita half-caste, chotara na kadhalika lakini kamwe si mweusi mwenzetu. Anakuwa mweusi anapofanikiwa na si wakati mwengine. Mbona hamjisifii Lewis Hamilton?

Tofauti na wewe mimi najivunia weusi wangu warts and all. Nyinyi mnajivunia kwa vile tu ameshinda urais, bila shaka mkitegemea kuwa ndio mmeukata! Mimi ushindi huu nauthamini kama unavyouthamini wewe lakini sitakubali unifanye nifungie macho mapungufu yetu. Weusi, Mkuu, si kuvaa beji ya Obama. Kama vile Obama mwenyewe alivyosema, uzalendo si kuvaa beji. Uzalendo ni zaidi ya hiyo. Ni kukipenda kitu pamoja na mapungufu yake.
 
Wakuu ninawaomba tuache kum beza Nyani. Kwa wale tulioanza hii safari tangia mwanzoni, mtakumbuka kwamba huyu bwana alikuwa mwenzetu..ninamaanisha alikuwa Democrat wa upande wa Hillary Clinton.
 
Nyani lazima achapwe mpaka asalimu amri tu, alizidi ngebe hapa.
 
Wakuu ninawaomba tuache kum beza Nyani. Kwa wale tulioanza hii safari tangia mwanzoni, mtakumbuka kwamba huyu bwana alikuwa mwenzetu..ninamaanisha alikuwa Democrat wa upande wa Hillary Clinton.

Capitol HIll nakubaliana na wewe, Nyani has been a good sport! Na mimi namtetea maana alituchangamsha sana! Ushabiki umeisha tuendelee na kazi zetu, unfortunately 🙂
 
inashangaza kuwa siasa inataka kuchukuliwa kama aina fulani ya uhasama kwamba aliyeshindwa basi asigidwe na kufanywa duni. Ndio maana viongozi wengine hung'ang'ania madaraka kwa sababu kushindwa ni fedheha wasiyoiweza. Obama kashinda, fair and square.

Walioshindwa wameshindwa na hilo ni fair and square. Sasa kukaa hapa na kuanza kunyosheana vidole na kukamiana ni kutokukomaa kidemokrasia.
 
Walioshindwa wameshindwa na hilo ni fair and square. Sasa kukaa hapa na kuanza kunyosheana vidole na kukamiana ni kutokukomaa kidemokrasia.


Ukimuuliza rafiki yangu Nyani atakwamba "miafrika ndivyo tulivyo" na wakati mwingine, ukiangalia mienendo yetu hata hapa kwenye forum, unashindwa kutokubaliana naye!!

Masanja: Nakubaliana na wewe. Hawa wenzetu wapo mbele sana na tuna mengi mno ya kujifunza kutoka kwao. Kitu kimoja cha kujifunza hapa ni kwamba kwa wenzetu uongozi ni utumishi, sio ulaji kama sisi, ndiyo maana ikitokea ameshindwa, anakubali mara moja na kumpongeza aliyeshindwa, maana kushindwa kwake sio mwisho wa maisha. Lakini kwetu mtu akishindwa anaweka makunyanzi hadi matakoni, na wakati mwingine yule anayeshinda anakuwa na nyodo kama unavyoshuhudia hapa, Mungu atusaidie!!
 
Masanja,

..hata mimi ile statement ya McCain ilinigusa kidogo. haswa haswa alivyoweza kuwatuliza washabiki wake waliokuwa na hasira ya kushindwa.

..zaidi, Mzee McCain amekubali kubeba mzigo wa lawama, kama upo, kutokana na kushindwa kwake.

..kwa Obama kwa kweli ni kama namtegemea atatoa hotuba nzuri siku zote. kwa kweli sikuwa overly impressed, it was almost a guarantee kwamba atashinda.

..ila ule umati kwa kweli was something different. ukisikia mtaji wa kisiasa basi ndiyo ule.

..kwa kweli tunamuombea heri ktk kazi yake ya kuiongoza Marekani na dunia. wako wanaodai kwamba Marekani ikipiga chafya, basi nchi nyingine hupatwa na nyu-monia.

Kitila Mkumbo,

..nadhani hata ile kukubali kushindwa tu, ni therapeutic in itself.

..ppl should concede defeat, and move forward with their lives, for their own good.

..hizo ngebe za washindi waachiwe wenyewe.

NB:

..kuanzia sasa mpaka January ambapo ataapishwa kwa kweli is just too long.

..nasubiri kwa hamu kujua nani atakuwa kwenye cabinet yake.
 

Nyani hakuwa anaongea siasa, ila alileta ngebe, kwa hiyo kwa sababu tunam mind ndugu yetu tunataka kumpa fundisho kuwa ngebe nyingi hazifai, na huwezi kumtukana mamba kabla hujavuka mto.

Nyani mimi nasubiri suti yangu, tailor made, usifikiri nimesahau au nitasahau.

Mkuu wangu Mch. najua anasubiri Carvoissier yake.
 



Iko siku utayala matapishi yako! Huo mfano (kauli) si wa kutumia kila unapojisikia.




.
 
Gottee,
Hivi unadhani Obama amefika hapa kwa sababu ya weusi wake au malezi aliyopewa? Tushangilie lakini tuwe humble enough kukiri mchango wa wengine!
 
O - Originally
B - Born in
A - Africa
M - Managing the
A - Americans
 
Jokaa Kuu

YOU SPOT IT.

Unajua wenzetu kuna vitu ambavyo wanaelewa fika kwamba ndivyo vinawafanya kuwa taifa. Kwa hiyo hawawezi kucheza navyo kamwe. Wamarekani wana arrogance zao lakini wanaheshimu sana katiba (founding document). Wanaamini kabisa maslahi ya taifa ni mbele siku zote. ni kama sisi ambavyo leo tunaanza kwa kujua au kutokujua kuchezea amani na mshikamano tulio nao kama taifa. My friend, na umaskini wetu.. tukipoteza hivi vitu..ndo utakuwa mwisho wetu kama taifa. Ofcourse inawezekana TANZANIA nyingine ambayo mimi na wewe hatutabahatika kuiona ikazaliwa.


......naimagine Supreme Court na Federal court zitajaa maliberals.....kama Stevens nadhani ataondoka Supreme Court....Duh..Conservatives kazi mnayo....

Whatever we do, kama alivyosema Kitila tuna mengi ya kujifunza kwa hawa watu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…