Pundit
JF-Expert Member
- Feb 4, 2007
- 3,733
- 141
whatchu talkn' bout Pundit?
Unajifanya umesahau siyo?
"There is a new Sheriff in town"
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
whatchu talkn' bout Pundit?
Unajifanya umesahau siyo?
"There is a new Sheriff in town"
Wakati sisi waafrika tunashangilia tukumbuke kuwa huyu mwana tulimtelekeza kama tulivyowatelekeza wengine. Yote haya ni matokeo ya malezi ya mama yake mzungu, bibi ( mungu aipumzishe roho yake mahali pema peponi), babu yake mzungu, baba yake wa kambo m-indonesia. Wakati huo sisi tulikuwa MIA kama tulivyo kwa mbegu zetu kibao tulizozitelekeza si ughaibuni tu bali hata hapo nyumbani. Ni mara ngapi sisi wanaume tumejitokeza bila aibu kudai damu yetu (ambayo tuliikana toka ikiwa tumboni hadi kuzaliwa) baada ya mzazi mwenzetu kuifikisha mahali ambapo tuna cha kujivunia? Tumekuwa mabingwa wa kuvuna tusichopalilia.
Wakati tunasherehekea inabidi tuone na aibu. Hasa sisi wanaume wa kiafrika! Mwanetu ametusamehe, inabidi na sisi tuonyeshe kuwa tunastahili msamaha huo!
Amandla.......
Nipo....kwa nini nikimbie? Maisha yanaendelea na tutapata fursa ingine 2012 na Bobby Jindal.....
Wakati sisi waafrika tunashangilia tukumbuke kuwa huyu mwana tulimtelekeza kama tulivyowatelekeza wengine. Yote haya ni matokeo ya malezi ya mama yake mzungu, bibi ( mungu aipumzishe roho yake mahali pema peponi), babu yake mzungu, baba yake wa kambo m-indonesia. Wakati huo sisi tulikuwa MIA kama tulivyo kwa mbegu zetu kibao tulizozitelekeza si ughaibuni tu bali hata hapo nyumbani. Ni mara ngapi sisi wanaume tumejitokeza bila aibu kudai damu yetu (ambayo tuliikana toka ikiwa tumboni hadi kuzaliwa) baada ya mzazi mwenzetu kuifikisha mahali ambapo tuna cha kujivunia? Tumekuwa mabingwa wa kuvuna tusichopalilia.
Wakati tunasherehekea inabidi tuone na aibu. Hasa sisi wanaume wa kiafrika! Mwanetu ametusamehe, inabidi na sisi tuonyeshe kuwa tunastahili msamaha huo!
Amandla.......
Bora umefika maana kidogo watu walitaka kuanza kutangaza kuwa Umechanganyikiwa kwa kushindwa hadi umepotea njia, eti uliingia nyumba ya jirani, ya kweli hayo?
Nataka nikuulize maswali wewe Muheshimiwa? BHO kwa kupata malezi ya mama/bibi yake mzungu na baba mu-indonesia amegeuka kuwa MZUNGU? Nataka nikuulize swali lingine. Hivi wanaotelekeza watoto ni watu weusi tu ikiwa na maana wazungu huwa hawatelekezi watoto?
Muheshimiwa kama BHO alitelekezwa na Baba yake sisi hayatuhusu! Hayo ni maisha yake binafsi na binafsi sijawahi kusikia AKILALAMA hadharani. Yanayotuhusu ni Historia aliyoaiandika huyu KIJANA! Kumbuka tukio hili limetokea baada ya miaka mingapi ya utabiri wa MLK!
BHO awe alitelekezwa au hakutelekezwa anabakia kuwa ni Mmarekani Mweusi Tii wa kwanza kuingia Jumba Jeupe hivyo basi na sisi binamu zake Waafrika Weusi Tii tunashangilia kuanzia huko huko kwa kina P Diddy, Senti Hamsini hadi huku Kegelo kwa kina Jaramogi na hata kule kusini kwa kina Zuma na kule Ufaransa kwa kina 'cheusi' Thuram hadi kule kwa kina Ze Mariaz LEO ni RAHA TUPU! Hayo ya kutelekezwa mfufue BHO Snr labda atakuomba radhi kwa niaba ya 'wazungu' wenzio (Bwa ha ha haaaa!) na atakuelewa na atakwenda kumuomba radhi BHO jnr! Vinginevyo kwa raha zetu tuache tusherehekee. Hapa nilipo kifuani kwangu nina Beji ina picha ya Obama ikiwa imeandikwa 'Obama'08 for President!' Nakatiza mitaa ya Kibena, Njombe! Hurrraaayyyyy!
Wakuu ninawaomba tuache kum beza Nyani. Kwa wale tulioanza hii safari tangia mwanzoni, mtakumbuka kwamba huyu bwana alikuwa mwenzetu..ninamaanisha alikuwa Democrat wa upande wa Hillary Clinton.
Walioshindwa wameshindwa na hilo ni fair and square. Sasa kukaa hapa na kuanza kunyosheana vidole na kukamiana ni kutokukomaa kidemokrasia.
inashangaza kuwa siasa inataka kuchukuliwa kama aina fulani ya uhasama kwamba aliyeshindwa basi asigidwe na kufanywa duni. Ndio maana viongozi wengine hung'ang'ania madaraka kwa sababu kushindwa ni fedheha wasiyoiweza. Obama kashinda, fair and square.
Walioshindwa wameshindwa na hilo ni fair and square. Sasa kukaa hapa na kuanza kunyosheana vidole na kukamiana ni kutokukomaa kidemokrasia.
Walioshindwa wameshindwa na hilo ni fair and square. Sasa kukaa hapa na kuanza kunyosheana vidole na kukamiana ni kutokukomaa kidemokrasia.
Ukimuuliza rafiki yangu Nyani atakwamba "miafrika ndivyo tulivyo" na wakati mwingine, ukiangalia mienendo yetu hata hapa kwenye forum, unashindwa kutokubaliana naye!!
Masanja: Nakubaliana na wewe. Hawa wenzetu wapo mbele sana na tuna mengi mno ya kujifunza kutoka kwao. Kitu kimoja cha kujifunza hapa ni kwamba kwa wenzetu uongozi ni utumishi, sio ulaji kama sisi, ndiyo maana ikitokea ameshindwa, anakubali mara moja na kumpongeza aliyeshindwa, maana kushindwa kwake sio mwisho wa maisha. Lakini kwetu mtu akishindwa anaweka makunyanzi hadi matakoni, na wakati mwingine yule anayeshinda anakuwa na nyodo kama unavyoshuhudia hapa, Mungu atusaidie!!