Yap! thatz true indeed. if an afrikan gene gets into any other race most definetely the baby will come out w/ black features i.e. big head, large nose, thick lips, curly hair, volumptuous body n ass (girls) etc.
Kuna mamilioni ya watu katika bara letu ambalo wanasubiri kwa hamu ushindi unaotarajiwa wa Obama kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi huko Marekani. Kuna tafrija na sherehe zilizoandaliiwa sehemu mbalimbali ambapo watu weusi watasimama kufurahia ushindi wa Obama.
Sitoshangaa wengi wanaosubiri huo ushindi wa Obama wanafanya hivyo si kwa sababu wanakubaliana na sera zake zote (kuongeza kodi, kugawanya utajiri n.k) au misimamo yake ya kijamii (kuunga mkono utoaji mimba au haki za mashoga n.k) bali wanafanya hivyo kwa sababu Obama ni "mweusi mwenzetu".
Hili hata hivyo linanikumbusha jinsi watu walivyomshabikia Kikwete mwaka 2005 licha ya kuwa hakuwa na rekodi yeyote, hakuwa tayari kufanya midahalo na wagombea wenzake na alikuwa na maneno matamu ya "change" yaliyotumiwa kwa mbiu ya "ari mpya, kasi mpya na nguvu mpya".
Wapo watu wale wale ambao leo wanamgeuka Kikwete ndio leo wanakumbatia kwa haraka maneno ya "change" na ya kuwa "Yes we can". Lakini nyuma ya ushabiki huu Watanzania na watu wa mataifa mengi ya dunia wanachoshabikia kule Marekani kwa kweli ni Rangi; kwamba hatimaye Taifa lenye watu wengi weupe likaongozwa na mtu mweusi!
hapa najikumbusha maneno ya Mwalimu "Sisi bwana hatutukuzi rangi, tunatukuza mtu bwana"!
Yawezekana ulimwengu ukakosea katika ushabiki wake wa Obama kama Watanzania asilimia 80 ya wapiga kura walivyokosea walipomshabikia Kikwete. Kweli Obama ataweza kutimiza ahadi yake ya "kuibadili Marekani, na kuibadili dunia"?
Yawezekana kiongozi ambaye watanzania na nchi za ulimwengu wa tatu zilipaswa kumshabikia ni McCain na siyo Obama kama wangeamua tu kuweka rangi pembeni? Well, masaa 24 yajayo will give us a clue.
Nimeshangazwa na tabia hii ya Waafrika wengi .Sijamsikia akiitaja Afika katika kampeni zake kabisa kabisa bali America American sasa watu wanacho komaa nacho ni kitu gani ? JK ndani ya USA wacha mtaona .
raisi obama...? No way, bado kabisa. President elect mccain......
Haya matatizo ya Mwanakijiji ya kuandika kina Makamba na siasa duni za CCM kila siku matokeo yake ndio haya ya kufikiri kila mtu anampenda/kushabikia Obama kwa sababu tuu ni mweusi,wewe endelea kuandika fantasy zako ili uendelee kupata attention,lakini sisi tunajua kwanini tuna support Obama..na ulivyo kuwa mwongo na uandishi wako style ya Mzalendo na Rai unazidi kutumia points za Joe the Plumber eti obama ataongeza kodi na kugawanya utajiri...
Ngoja nikupe hint why i support Obama..possibility ya 50yrs of cuban embargo inaweza kuwa history!
Kuna mamilioni ya watu katika bara letu ambalo wanasubiri kwa hamu ushindi unaotarajiwa wa Obama kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi huko Marekani. Kuna tafrija na sherehe zilizoandaliiwa sehemu mbalimbali ambapo watu weusi watasimama kufurahia ushindi wa Obama.
Sitoshangaa wengi wanaosubiri huo ushindi wa Obama wanafanya hivyo si kwa sababu wanakubaliana na sera zake zote (kuongeza kodi, kugawanya utajiri n.k) au misimamo yake ya kijamii (kuunga mkono utoaji mimba au haki za mashoga n.k) bali wanafanya hivyo kwa sababu Obama ni "mweusi mwenzetu".
Hili hata hivyo linanikumbusha jinsi watu walivyomshabikia Kikwete mwaka 2005 licha ya kuwa hakuwa na rekodi yeyote, hakuwa tayari kufanya midahalo na wagombea wenzake na alikuwa na maneno matamu ya "change" yaliyotumiwa kwa mbiu ya "ari mpya, kasi mpya na nguvu mpya".
Wapo watu wale wale ambao leo wanamgeuka Kikwete ndio leo wanakumbatia kwa haraka maneno ya "change" na ya kuwa "Yes we can". Lakini nyuma ya ushabiki huu Watanzania na watu wa mataifa mengi ya dunia wanachoshabikia kule Marekani kwa kweli ni Rangi; kwamba hatimaye Taifa lenye watu wengi weupe likaongozwa na mtu mweusi!
hapa najikumbusha maneno ya Mwalimu "Sisi bwana hatutukuzi rangi, tunatukuza mtu bwana"!
Yawezekana ulimwengu ukakosea katika ushabiki wake wa Obama kama Watanzania asilimia 80 ya wapiga kura walivyokosea walipomshabikia Kikwete. Kweli Obama ataweza kutimiza ahadi yake ya "kuibadili Marekani, na kuibadili dunia"?
Yawezekana kiongozi ambaye watanzania na nchi za ulimwengu wa tatu zilipaswa kumshabikia ni McCain na siyo Obama kama wangeamua tu kuweka rangi pembeni? Well, masaa 24 yajayo will give us a clue.
Obama is the 44th President of the USA.JUST CONFIRMED AFTER JUST WINNING CALIFORNIA
...ilikuwa haina hata haja ya kumjibu!! Obama ni baaaaaab'kubwa kuliko Nyerere mara million!!!
Mzee Mwanakijiji,
Kwanza Obama si Kikwete!
Obama hajatuhumiwa na hajatumia fedha chafu kugombea uraisi wa Marekani kama Kikwete na CCM walivyofanya.
Furaha ya watu Weusi, mimi nikiwa mmoja wapo ni kule kuushinda Unyonge uliojengwa ndani yetu, ule wa Nyani wa Ngabu kusema ndivyo tulivyo, unyonge wa kuonekana kuwa hatuna thamani wala uwezo wowote.
Ushindi wa Obama si kwa watu Weusi na Waafrika tuu, bali ni kwa kila mtu ambaye siku zote amelelewa na kukuwa katika mazingira yanayomwambia kuwa yeye ni batili, nusu na hana thamani.
Ushindi wa Obama ni sawa na kuvunja minyororo ya utumwa na ukoloni. Pamoja na kuwa ni kweli kuwa si yeye pekee ambaye ataongoza nchi ya Marekani, lakini kitendo cha yeye kuwashinda wale ambao siku zote wamekuwa wakidharau na kukandamiza binadamu wa rangi, dini, jinsia na aina nyingine kwa kujifanya wao ndio wateule, ni dalili tosha kuwa nyakati zinabadilika na kila tunaloambiwa haliwezekani, linawezekana.
Ushindi wa Obama naupokea kama siku Chadema, CUF, TLP au chama kingine kinaposhinda Ubunge nchini Tanzania au siku mojawapo ya Vyama hivi au kwa umoja vitaing'oa CCM kutoka madaraka ya kututawala Watanzania.
Najua una mtazamo wako wa kulia ambao ni tofauti na ule wa Obama kisera na hata labda kiimani, lakini ukweli unabakia kuwa tulishaambiwa haitawezekana, hamuwezi, sasa milango imefunguka, tumeona na kushuhudia kuwa inawezekana, tunaweza na zaidi tuna haki sawa.
Huu ni mwanzo wa mwisho wa Unyonge. Hata kama hataweza tatua matatizo yote au kuleta Maisha bora kwa kila Binadamu au Mwananchi na mkazi wa Marekani, kuweza kupata ushindi na kuwa mshindi ni tuzo ya pekee na ni tumaini na faraja ya ajabu kwa kila ambaye amedhalilishwa na kufanywa mnyonge.
Alichuma juani na sasa ana haki ya kulia kuvulini.