Furaha ya watu Weusi, mimi nikiwa mmoja wapo ni kule kuushinda Unyonge uliojengwa ndani yetu, ule wa Nyani wa Ngabu kusema ndivyo tulivyo, unyonge wa kuonekana kuwa hatuna thamani wala uwezo wowote.
Ushindi wa Obama si kwa watu Weusi na Waafrika tuu, bali ni kwa kila mtu ambaye siku zote amelelewa na kukuwa katika mazingira yanayomwambia kuwa yeye ni batili, nusu na hana thamani.
Ushindi wa Obama ni sawa na kuvunja minyororo ya utumwa na ukoloni. Pamoja na kuwa ni kweli kuwa si yeye pekee ambaye ataongoza nchi ya Marekani, lakini kitendo cha yeye kuwashinda wale ambao siku zote wamekuwa wakidharau na kukandamiza binadamu wa rangi, dini, jinsia na aina nyingine kwa kujifanya wao ndio wateule, ni dalili tosha kuwa nyakati zinabadilika na kila tunaloambiwa haliwezekani, linawezekana.
Acha undumilakutatu! Kila unapopata nafasi ya kukanyaga race yangu kwa madai kwamba haina thamani unairukia kwa kila aina ya kejeli, kashfa na matusi kuonyesha imekosa utashi wa kuitwa ya watu.
Posted by Rev. Kishoka:
``Mjaluo wetu anachechemea, yuko hoi bin taaban, kathibitisha maneno ya Nyani
"ndivyo Tulivyo" ngoja nikamdai refund ya mchango wangu kama Kikwete na BAE! ´´
Posted by Rev. Kishoka:
´´visa hivi vinaelemea sana kumuonyesha kuwa kauli ya
"Ndivyo Tulivyo" ina uhalali!
Posted by Rev. Kishoka:
´´Siku moja, Mwafrika, Mwarabu, Mwasia na Mzungu walikuwa kijiweni, Mungu akaja akawaambia nina vitu vinne inabidi niwagawie, kubalianeni nani anataka nini. Vitu hivyo vilikuwa ni Utajiri, Maarifa, Biashara na Ngoma.
Mzungu akadamka, mimi nataka Akili...
Mwafrika akakimbilia ngoma yake akaikumbatia akaanza kutumbuiza huku Mzungu akitafakari nini cha kufanya, Mwarabu akiufurahia utajiri wake na Mwasia akipanga mipango ya biashara!
Mpaka leo tumeendela kukumbatia Ngoma na ndio maana tu mahiri kwenye sanaa!
... ni ile laana ya mtoto wa Nuhu (aliyejenga safina)aliyemcheka baba yake kuwa uchi baada ya kulewa. Mchungaji akatuambia kuwa uzao wa
yule mtoto aliyelaaniwa ndio chimbuko la Waafrika na sisi ni watu tuliolaaniwa kuwa watumwa na watumishi wa wenzetu! ´´
Posted by Rev. Kishoka:
´´Nyani Ngabu kasema,
Ndivyo tulivyo, kauli mbiu hiyo inaelekea kuwa ni kweli kila siku!´´
Posted by Rev. Kishoka:
´´Saidia Maskini, saidia baba!
Ndivyo Tulivyo!´´
Posted by Rev. Kishoka:
´´Nyani,
Tulishapigwa Limbwata na Mkoloni kuwa
sisi ni Uzao wa Kaanani, mtoto wa Ham ambaye alipewa laana ya milele na Babu yake Nuhu kuwa tutakuwa watumwa!...ni laana hizo
ndio maana tuna nywele Kipilipili!´´
Posted by Rev. Kishoka:
´´Wee Nyani, mbona huachi ujinga
😉 Yaani you made me believe for a minute
Ndivyo Tulivyo!´´
Posted by Rev. Kishoka:
´´The fact that we are allowing all these foreign companies to come and operate in Tanzania and provide them with "healthy" accomodations such as 5-10 years Income and Tax Break, in addition to other "incentives" to plush the red carpet fibre so they can walk like emperors to rescue Tanzania from its own failures, is enough to acknowledge that
Ndivyo Tulivyo na
ni Wajinga waliwao! ´´
Posted by Rev. Kishoka:
´´Nyani,
Ndivyo tulivyo.
Tunashindwa kufanya self examination ya mioyo yetu na kuanza kujituma na tunakimbilia misaada maana ndio njia fupi kwa kuwa hatutaki kufanya kazi kwa bidii na kujituma ili tukishachuma juani, tule kivulini.´´
Posted by Rev. Kishoka:
´´You are being too dismissive without even making a single effort to try if option presented at the table could work. Huu ndio what Nyani Ngabu calls
"ndivyo tulivyo"! ´´
Posted by Rev. Kishoka:
´´Tumechoka kusubiri na kukumbushwa na Nyani Ngabu kuwa
ndivyo tulivyo, tunaanza wote kushiriki katika ujenzi wa Taifa kwa hali, mali na fikra.´´
Posted by Rev. Kishoka:
´´yes ndivyo tulivyo!´´
Posted by Rev. Kishoka:
´´Swali ni lini tutaacha kulaumu na kuishi kama "ndivyo tulivyo" na kuleta mabadiliko? je wewe uko tayari kuanza mabadiliko ambayo Nyani anayadai kama Tomaso ndipo aamini kwa kuanza badili mwenendo wako wa kuonekana
"ndivyo ulivyo"?´´
Rev. Kishoka, unapataje balls za kuiambia race yangu "ndio maana tuna nywele kipilipili"?