Rais Museveni ‘amsuta’ mlimbwende kwa kuvaa wigi

Rais Museveni ‘amsuta’ mlimbwende kwa kuvaa wigi

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
Rais wa Uganda Yoweri Museveni amekutana na mlimbwende wa nchi hiyo ambaye hivi majuzi ameshinda taji la mlimbwende bora wa Afrika.

Quiin Abenakyo alitawazwa kuwa Miss Uganda mwezi Agosti na kushiriki shindano kubwa la ulimbwende duniani la Miss World nchini Uchina mwezi huu ambapo aliingia kwenye tano bora na kutawazwa taji la Miss Africa.

Bi Abenayako amerejea Uganda jana, na saa chache baadae akaenda Ikulu kukutana na rais Museveni.

Rais Museveni alimsifia mlimbwende huyo na waandaji wa shindano la Miss Uganda na kuahidi kuwapa ushirikiano. Lakini hata hivyo ‘alimsuta’ mrembo huyo kwa kuvaa “nywele za Kihindi”.

Abenakyo ni mrefu haswaa, binti mrembo kutoka Musoga. Tatizo langu pekee ni kuwa alikuwa amevaa nywela za Kihindi. Nimemsihi kubaki na nywele zake za asili. Lazima tuuoneshe uzuri wa Kiafrika katika uhalisia wake,” ameandika Museveni kupitia ukurasa wake rasmi wa Twitter.


Abenakyo is indeed a tall, beautiful Musoga girl. My only concern is that she was wearing Indian hair. I have encouraged her to keep her natural, African hair. We must show African beauty in its natural form.​
Ujumbe huo wa Museveni umeibua mjadala nchini Uganda ambapo watu wengi wanamuunga mkono kutaka wasichana kuacha mawigi. Hata hivyo kuna kundi kubwa la watu ambao wamechukuli kauli hiyo ya museveni kama kichekesho.

Museveni anajulikana kwa kuongea kile atakacho bila kujali maoni ya watu yatakavyokuwa dhidi yake.

_104889473_7.jpg

Mkutano wa wawili hao ulifanyika katika Ikulu ya Entebbe. Museveni alimpongeza mrembo huyo kwa kumaliza masomo yake ya shahada hivi karibuni akisema kuwa mlimbwende huyo ni: “kielelezo cha msemo wa uzuri uliombatana na akili.”
 
Namkubali sana rais mseveni...

Sema afuate utaratibu wa kuachiana madaraka.

Back to the topic..
Asingevaa nywele za mtumba angependeza sana huyo mdada.
 
Safi sana.

Huwa nawashangaa wanaowachaguwa, labda kuwa fake ni kigezo cha urembo?
Kwenye mashindano hayo hawaangalii tu sura na muonekano. Wanaangalia akili ya mlimbwende na mengineyo
 
Kama kigezo cha urembo ni akili basi kwa wema waliangalia tahira
 
Akili kivipi? Kwahiy unataka kuniambia Wema Sep aliangaliwa akili gani?
Siongelei miss Tanzania hapo nilivyomjibu. Naongelea miss world ambayo huyo miss Uganda kashiriki. Uzuri peke yake sio kigezo cha ushindi kulikua na mambo mengine yanayowaingiza washiriki kwenye top 30 na mpaka top 5. Ikiwemo ujibuji wa maswali ambao kilaza lazima atoke kapa, michezo, ubunifu etc.
Na kuhusu wema sepetu ebu rudi kwenye miss Tanzania 2006 uone top 5 maswali waliyoulizwa na majibu yao then pambanua mwenyewe
 
Namkubali sana rais mseveni...

Sema afuate utaratibu wa kuachiana madaraka.

Back to the topic..
Asingevaa nywele za mtumba angependeza sana huyo mdada.
m7.jpg

Huyu mtoto wa Museven nahisi huyu jamaa Mnyarwanda watoto wake wanafanana na wakagame
 
Back
Top Bottom