DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amezitaka wizara zinazoshughulika na biashara kutoka Tanzania Bara na Visiwani kuhakikisha kuwa wazalishaji wote wa bidhaa nchini wanatumia nembo ya “Made in Tanzania.” Lengo la hatua hiyo ni kuongeza utambulisho na ushindani wa bidhaa za Tanzania katika masoko ya kimataifa.
Dkt. Mwinyi alitoa agizo hilo jijini Dar es Salaam wakati akifungua rasmi Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), sambamba na uzinduzi wa nembo maalum ya biashara inayotambulisha bidhaa za Kitanzania.
Amesisitiza kuwa kila mzalishaji wa bidhaa nchini anapaswa kutumia nembo hiyo kwenye vifungashio au mawasiliano yao ya kibiashara, ili kusaidia kuitangaza Tanzania ndani na nje ya nchi, na kuzifanya bidhaa zitambulike kimataifa.
Aidha, Dkt. Mwinyi ameipongeza Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) kwa ubunifu wao na juhudi za kuboresha maonesho hayo kila mwaka, na kuongeza ushiriki wa kimataifa. Ametoa mfano wa Japan, ambapo bidhaa nyingi za Kitanzania zimekuwa zikivutia wateja kutokana na ubora wake, na kuwahamasisha Watanzania kuendelea kujifunza na kuboresha bidhaa zao kwa viwango vya kima
taifa.