Rais Mwinyi asema atabeba gharama zote za Uwanja wa Amaan katika Fainali ya Simba Vs RS Berkane

Rais Mwinyi asema atabeba gharama zote za Uwanja wa Amaan katika Fainali ya Simba Vs RS Berkane

RAIS DKT. MWINYI ABEBA GHARAMA ZOTE UWANJA WA AMAAN COMPLEX MECHI YA SIMBA DHIDI YA RS BERKANE

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ametoa Zawadi Maalum kwa timu ya Simba Sports Club kwa kugharamia matumizi ya Uwanja wa New Amaan Complex bila gharama yoyote kwa ajili ya kucheza fainali ya pili ya Kombe la Shirikisho la CAF, itakayofanyika siku ya Jumapili, tarehe 25 Mei 2025, saa 10 jioni.

Uamuzi huo wa Rais Dkt. Mwinyi unalenga kudhihirisha mapenzi yake ya dhati kwa michezo pamoja na kuhamasisha ushindi kwa timu ya Simba SC, katika mechi hii ya kihistoria dhidi ya RS Berkane kutoka Morocco. Hatua hiyo pia ni sehemu ya juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar za kuunga mkono maendeleo ya michezo na kuleta hadhi ya kimataifa.

Mbali na kuruhusu matumizi ya Uwanja huo bure, Rais Dkt. Mwinyi amechukua dhamana ya kugharamia maandalizi yote muhimu ya uwanja kwa mechi hiyo.

Aidha, fainali ya mechi hiyo inatarajiwa kuhudhuriwa na maelfu ya washabiki kutoka ndani na nje ya nchi.

Kwa kutambua uzito wa mechi hiyo kwa Taifa, Rais Dkt. Mwinyi ameahidi kuhudhuria fainali hiyo sambamba na Watanzania wote katika kuwaunga mkono Simba SC na kuhamasisha ushindi wa kihistoria.
Maelfu ya mashabiki wataingiaje kauwanja kadogo vile?
 
Atabeba yeye!!!!

Itabeba Selikali ya mapinduzi Zanzibar ( SMZ )
Kupitia kodi za Walala hoi???????

HUKU TANGANYIKA WATU WAMEANZA KUAMKA HAWAPENDI UPUMBAVU.
 
Tanzania ni kigeu geu kupita kiasi..........kumbuka kuna watu waliuza tiketi ...........hivi huwa inakuwaje maana ehh

Nadhani kilichotolewa bure kwa Simba ni gharama za matumizi wa uwanja (event fee) na sio mashabiki kuingia bure, soma vizuri hii nukuu...

Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ametoa Zawadi Maalum kwa timu ya Simba Sports Club kwa kugharamia matumizi ya Uwanja wa New Amaan Complex bila gharama yoyote kwa ajili ya kucheza fainali ya pili ya Kombe la Shirikisho la CAF.
 
Kama ni la nje ya nchi bard ila kama ni hapa hapa noo staki mpaka niwe na uhakika wa kazi wizarani
Kazi wizarani una back up Kijana? Serikalini mtu anaitwa Neema lakini jina alilopewa na wazazi wake ni Sikitu 🤣

Kama una backup Inshallah you will make it 🤷
 
Kuna wakati naona Simba hata akipoteza hili kombe sawa. Wanasiasa wanataka kutumia Simba kueneza siasa zao. Cha ajabu, akishinda badala washukuriwe wachezaji na benchi ufundi utasikia anashukuriwa Rais.

******* sana
 
Hao wameshalizwa tayari, Kuna watu wailipia ya mkapa, na wakalipa tena ya Amaani, sasa imetangzwa Bure. Hzo pesa zinarudije na haliyakua Simba itapatiwa pesa kama mauzo kutoka kwa Raisi.
Sidhani kama kuna tiketi ya bure.
Yeye atagharamia malipo ya uwanja pamoja na maandalizi mwngine ila mashabiki kuingia uwanjani kila mmoja ajilipie
 
Baada ya lengo lake la Visit Zanzibar kufanikiwa sasa kaamua awapake mafuta koloizdad kwa mgongo wa chupa.
 
Hao wameshalizwa tayari, Kuna watu wailipia ya mkapa, na wakalipa tena ya Amaani, sasa imetangzwa Bure. Hzo pesa zinarudije na haliyakua Simba itapatiwa pesa kama mauzo kutoka kwa Raisi.
Wapi wamesema itakuwa bure?
 
Back
Top Bottom