Rais Mwinyi atoa onyo kwa watakaopandisha bei ya bidhaa Zanzibar


Ama kwa hakika Dr Mwinyi nampa heko sana ktk uongozi wake
Anaonyesha kujali maslahi mapana ya wananchi wake anaowaongoza

Kila kukicha huwa napenda kumfatilia na kumsikiliza, yuko njema sana

Naiomba na kuisihi sana CCM huyu MamΓ‘ yetu aishie 2025 tu, kisha Dr Mwinyi aje Bara
 
Huyu mwinyi nae anajitutumua tu..hajui Tanganyika huku rais kasema vitu lazima vipande bei kwa sababu ya vita..yeye anampinga chui jike.

Soon ataitwa dodoma kwenye kamati ya maadili anapingana na kauli ya rais wa JMT.

#MaendeleoHayanaChama
 
Huku kwetu biambiliki kasema tutegemee vitu kupanda bei sababu ya vita yani ata huo mchele tunaolima humu ndani. Kabla ya magu kufa mbolea ilikuwa 50000-54000 alipoingia huyu145000 sababu ya vita imeongezeka 5000 nakuwa 150000.mama wa hovyo sana .
 
Kiufupi hii nchi bi ambiliki imemshinda!!!
 
Wakati wa Huko anawaambia Wananchi wake hivyo, ye wa huku anaawaambia Watendaji wake watueleze ukweli kua kupanda Kwa Bei hakuepukiki.
 
Huyu bibi yenu ni mnafiki na hana mafanikio yoyote toka aingie zaidi ya wananchi kuishi kwa jasho na damu
Mfanikio anayo makubwa sana,
Kwenye kuchamba na kusuta watu amefanikiwa sana
 
Ni muda wa mimi kurejea nyumbani najua hata , Bibi kule Jango'Mbe kanimisi sanaπŸ™
 
Zanzibar ni ndogo kuliko Dar es Salaam,
Mbara wetu anawapambania wanzanzibari kule visiwan ila huyu wa. Kwetu anapambana kuhakikisha kuwa tutapata tabu san
 
wakati wa kwetu amekazania kusema bidhaa zitaendelea kupanda, nchi yetu bidhaa zinauzwa bei ndogo kuliko nchi zingine, kwahiyo tujiandae kupanda kwa bidhaa hapa nchini kisababishi kikubwa ni vita ya urusi na ukraine.. Mwenzake wa zanzibar anasema bidhaa zisipande kwa kisingizio cha vita ya ukraine na urusi. Ama kweli kuna tofauti kati ya ME na KEπŸ™„
 
Huu wimbo kila mwaka unaimbwa imekuwa kama routine. Impact yake haionekani. Isitoshe urais wa Zanzibar na Ramadhan vina uhusiano gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…