Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema ana matumaini makubwa kuhusu mafanikio ya mchakato wa maridhiano kutokana na dhamira ya Wananchi ya kuona amani, umoja na mshikamano vinaendelea kudumu Nchini.
Dkt. Mwinyi amesema moja ya sababu zinazompa matumaini ni kuona kuwa Wananchi wengi wa Zanzibar na Tanzania Bara wanaunga mkono maridhiano na wanathamini utulivu wa kisiasa kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.“Sababu nyingine inayonipa matumaini ni kubaini kuwa wananchi wengi wa Zanzibar na Tanzania Bara wanataka maridhiano na ni Waumini wa amani, umoja na mshikamano