Leak
JF-Expert Member
- Feb 22, 2012
- 52,916
- 43,505
Mh Rais mashitaka dhidi ya Mbowe na wenzake yanashitusha sana watu wengi na hata wale ambao kwa vyovyote si mashabiki wa Mbowe au CHADEMA na ni mashitaka ya juu sana mtu kutuhumiwa nayo hasa mtu wa karba ya Mbowe kwa hiyo matarajio yetu ni kuwa serikali na DPP walishajipanga kumpeleka Mh Mbowe Mahakamani kesho jumatatu.
Na litakuwa jambo la busara sana kama mtamuachia huru Mbowe kama mtashindwa kumpeleka kesho Mahakamani ili mkajipange upya.
Mh Rais lazima utambue tuhuma dhidi ya Mbowe ni tuhuma hatari sana ambazo Serikali itapaswa kuthibitisha pasi na shaka au kesho aachiwe huru.
Kuendelea kumshikilia Mbowe kutaendelea kuthibitisha kuwa kuna shida nyingine kwa DPP na Jeshi la Polisi.
Mh Rais na DPP mnapaswa kuionesha dunia kuwa mnatenda haki kwa kumpeleka Mbowe Mahakamani kesho au kumuachia huru.
Waslaaam