SI KWELI Rais na mfadhili wa Mighty wanderers fc ajiuzulu baada ya kufungwa na simba

SI KWELI Rais na mfadhili wa Mighty wanderers fc ajiuzulu baada ya kufungwa na simba

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
kumekuwa na chapisho linalodai kuwa rais na mfadhili wa mighty wanderers fc, dkt. thomson mpinganjira, amejiuzulu nyadhifa zake ndani ya klabu hiyo baada ya kukerwa na kiwango cha timu katika mchezo wa ligi ya mabingwa afrika dhidi ya simba sc.

Rais na Mfadhili wa klabu ya Wanderers FC, Dkt. Thomson Mpinganjira, amejiuzulu nyadhifa zake kw.jpg
 
Tunachokijua
Kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii kumekuwa na chapisho linalodai kuwa rais na mfadhili wa Mighty Wanderers FC, Dkt. Thomson Mpinganjira, amejiuzulu nyadhifa zake ndani ya klabu hiyo baada ya kukerwa na kiwango cha timu katika mchezo wa ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya Simba SC.

Chapisho hilo pia linadai kuwa Mpinganjira, kupitia barua ya kujiuzulu, alieleza kusikitishwa na kiwango cha wachezaji na benchi la ufundi, akimkosoa kipa wa timu pamoja na maamuzi ya kocha kwa kushindwa kufanya mabadiliko ya kimkakati kwa wakati.

Ufuatiliaji umebaini kuwa hakuna ushahidi wa kuaminika unaothibitisha kuwa Dkt. Thomson Mpinganjira amejiuzulu nafasi zake ndani ya Mighty Wanderers FC kutokana na matokeo au kiwango cha timu dhidi ya Simba SC.

Katika hatua nyingine ukurasa rasmi wa klabu ya Mighty wanderers umekanusha Taarifa hizo huku ikisema kuwa Taarifa hizo ni potoshi

Vilevile, chombo cha habari cha Malawi Freedom Network, kimeripoti kuwa mmiliki huyo wa klabu amekanusha taarifa hizo, akisema kuwa kwa sasa hana mpango wa kuondoka katika klabu hiyo kwa sababu ya matokeo yaliyopatikana.

Pia katika hatua nyingine amesema kuwa ataendelea kuwa mfadhili wa timu.

Aidha ufuatiliaji zaidi umebaini kuwa Poster iliyotumika ikiwa na utambulisho wa chombo cha habari cha Kitenge ni ya kubuni na haijachapishwa na chanzo hicho.
Back
Top Bottom