Rais ni Muislamu, walio chini yake nao pia na Dini zao. Siri ni moyoni mwake Rais. Tunahitaji Brand ya Taifa sio vinginevyo

Shocker

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2012
Posts
2,175
Reaction score
4,181
Serikali za Tanzania zinakumbatia wanaoendeleza ugahaba na ushenzi, na wanamuziki wote hapa Tz ukifuata mienendo yao hawana isipokuwa kuendeleza tabia chafu, mambo ya haramu kwao wao wanayafanya kuwa halali na wengine huvuka mipaka na kuzichanganya dini kati tabia zao za ufuska.

Mambo yao yalipofikia huwezi kukaa na familia yako ukiwaangalia kwenye TV ni aibu na fedheha kwenye jamii.

Viongozi wa dini haifai kabisa kuwajadili watu hawa wacheni wapuuzeni kwani kushirikiana nao ni kuzipotosha dini,watu hawa hawana nafasi katika dini, msimamo ni kitu muhimu sana, viongozi wa dini wanawatoa waumini katika misimamo, utakuta wakuu hawa wa ufuska wakitoa misaada, kujenga misikiti makanisa kusaidia watoto , kwa ufupi ni kuipiga na chini misaada yao yote kwa maana ya kuikataa mchana kweupe ,hizi dini zilikuwepo kabla mama zao na baba zao hawajazaliwa na zitaendelea kuwepo bila ya hata kutumia ndururu yao..

Wao weshaangami wasitake kumsaidia Shetwani kuzidi kuwapoteza wengine.

Nikirudi mitaani kuna ngoma ambazo utawaona wadodo wadogo sana wakihemkwa kupita maelezo tuseme wanawashinda mama zao, mambo ambayo hupelekea kushughulikiwa wakiwa wadodo, kisha utasikia wazee wao wakipiga makelele mtoto wao kabakwa,sijui kwanini hawashangilii kwa kupata aliyoyalima ,yaliyomkuta mwana wao ni mavuno.

Hawa washezi wanamuziki walio yaani hawana tofauti na kaumu zilizoangamizwa leo wanasimama kwenye shughuli za kitaifa ,Tunasema Tanzania haina dini ila wananchi wake wana imani tofauti kinachotakiwa ni kuheshimiana ,mnajua Rais dini yake na mnajua waliochini yao wana dini zao na ndio ikawepo brass band ya Taifa inayotoa burudani zisizo na aibu wala viashiria vya kuaibisha.

Leo Tanzania wakija au wakifikiwa na wageni wa kiserekali kubwa ni kupelekwa wakata viuno pale uwanja wa ndege na kule jeshini nako Raisi akiwa kwenye maadhimisho yao wanaletwa wakata viuno ndio panoge ,hivi jeshini hakuna brass band ya kutumbuiza ? Ni aibu na kuwadhalilisha jamii ya wanawake akiwemo Raisi ,hivi yakatapwo mauno Rais anawatazamaje walio pembeni yake ya wanaosisimkwa na mwili ? Ni fedheha japo utamuona Rais haridhiki hubaki kumeza mate tu ,Je hawezi kuwaita pembeni na kuwaeleza niwapo baadhi ya mambo sipendi kuyaona sio mazuri kwa kioo cha jamii ,awambie hilo tu watamfahamu na wao watayarishaji watamfahamu.
 
Ngoma na muziki kwa ujumla ni ujinga ..Watu wajidhalilisha kabisa ,unakuta mtu anajielewa ila akifika huko ukumbini kwenye mziki anafanya mambo ya kijinga ,wale wacheza ngoma kichwani hamna kitu kabisa.

Ukija kwa hao wasanii , wanajifanya muda mwingine wanajua dini ,kama Mwijaku na Manara ila ni washenzi tu ..Hawa walitakiwa wapigwe marufuku kwenye ishu za kidini ,Mwijaku leo anamsema mtu kuhusu dini kesho unamuona mwanae anatembea nusu uchi yaani tabu na huyo Manara ana miaka 50 ila hata ndoa anafanya mchezo ,anaona na kuacha ni ujinga tupu.
 
Yule waziri wao kutoka Madudu Kilosa mwenye jina lisiloeleweka ni la imani gani mpenda Singeri ndiyo kichocheo cha yote hayo
 
Hiyo wizara wangempa Kangi Lugola awe anashinda anakatika nao
 
Watu mmechafukwa, ikifika 2030 watu tutaanza kugawana fito.
 
Unachekesha mkuu, hivi kuna sheikh yeyote mwenye ubavu wa kukataa hela haramu hapa nchini, tutajie. Njaa ni kitu kibaya sana, we angalia wasanii wetu hawa wa bongo movie hususani mademu walivyo na njaa na kuhaha huku na kule kutafuta wanaume wa kuwaweka mjni mpaka wanasikitisha na ndivyo ilivyo kwa masheikh.
 
Nchi haina dini japo watu wake wana dini. Heri hao washenzi ni mambo yao binafsi kuliko huyu muislam wenu anayeibia nchi mchana kweupe hata kututukana na kutuita machawa.
 
Hiyo wizara wangempa Kangi Lugola awe anashinda anakatika nao
Kangi sidhani kama ni mtu sahihi kwa hii wizara, mtu anayefaa pale ni yule mbunge anayepiga serekasi bungeni na kuangalia sinema za ngono huku wenzake wakijadili bajeti.
 
Kuna tatizo gani watu kukata viuno??
 

Brand Band ndiyo nini hii​

 
Kuna tatizo gani watu kukata viuno??
Hivi mwanao wakike anaweza kukukatia viuno mbele yako ,tuchukulie amekwisha olewa ,baba yake upo hapo unaangalia TV anakuja yeye anakukatikia na kibwebwe anajifunga ,utakuwa na tatizo ?

Nimepata ujumbe ,kutoka mamlaka husika wanasema wameshanifahamu .
 
Mbona husemi CCM iache kutegemea polisi?
CCM haitegemei polisi itakuwa hamjagundua tu kuna kaufa fulani wanakitumia hata CHADEMA majuzi kule mbeya walisema watakitumia kuwakamata wanasiasa wa CCM saa za usiku au kwenye mabaa.
 
Kiongozi muislamu yoyote awezi kuwa na akili huu ni ukwelu uliotukuka hakuna muislamu anaweza kubisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…