Rais ni sehemu ya Bunge; inamaanisha ndiye Mkuu wa Bunge?

Rais ni sehemu ya Bunge; inamaanisha ndiye Mkuu wa Bunge?

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
104,319
Reaction score
183,639
Kuuliza siyo ujinga.

Mosi Rais ni sehemu ya Bunge naomba kuelimishwa maana yake kisheria zaidi.

Pili naomba kuelimishwa tofauti ya Parliament na National Assemby kisheria zaidi.

Ramadhan Kareem.
 
Kwa uraia wa darasa la tatu, bunge lina sehemu mbili, sehemu ya kwanza ni Raisi na sehemu ya pili ni Wabunge.

Wabunge waliozidi theluthi mbili ya jumla ya wabunge wote wanaweza kupiga kura ya kutokuwa na imani na raisi.

Raisi anaweza kulivunja bunge kabla wabunge hawajapiga kura hiyo.

Raisi akigoma kusaini mswaada kwa mara tatu, bunge linavunjika.

Kwahiyo kimsingi, bunge halina uwezo wa kumtoa raisi madarakani ila raisi anaweza kulivunja bunge.

Sasa, kutoka hapo kwenye darasa la 3 kuna madarasa mengi mengi juu mpaka uprofesa, naimani wajuu zaidi watajazia/kuweka sawa kitaaluma zaidi
 
Halafu tunaimbiwa ni mhimili unaojitegemea[emoji1787]
Bunge linazinduliwa na Rais na linavunjwa na Rais, mikutano ya bunge huarishwa na PM na siyo Spika, pia PM na mawaziri ni wabunge.
 
Back
Top Bottom