Uchumi wa Kati
Member
- Jul 3, 2020
- 29
- 63
Zaidi ya miaka 40 shule hii ya msingi Mpakani iliyopo kata ya Mabibo mkoa wa Dar es Salaam kujengwa chini ya nyaya za umeme mkubwa wa gridi ya Taifa hali inayohatarisha maisha ya wanafunzi, maana nyaya ikikatika lazima maafa makubwa yatokee
Simu za nyuma Tanesco walivunja nyumba zilizopo ndani ya mita 30 ndani ya eneo la TANESCO na kuiacha shule
Inasemekana enzi za mbunge wa Kinondoni shule hii ilitengewa eneo maeneo ya Garments karibu na Chuo cha Usafirishaji Mabibo, hata hivyo eneo hilo limeuzwa na wajanja waliokuwa na madaraka kwa mtu binafsi.
Shule hii ni miongoni mwa shule nyingi zilizojengwa enzi za mbunge wa Kinondoni katika utawala wa Nyerere. Mbunge huyo alikuwa anaitwa Bryson.
Hivyo kupitia waziri wa Ardhi namuomba Mhe. Rais afuatilie maeneo yote ya serikali yaliyouzwa kwa watu na viongozi wasio waaminifu.
Tunajua Mhe. Rais were ni mfuatiliaji na kiongozi makini, tunu ya Taifa. Jambo hili naamini utalishughulikia kabla ya kuapishwa kwa Mara ya pili kuongoza Taifa letu.