Rais Putin afanya ziara ya kushtukiza Mariupol Ukraine na Crimea

Rais Putin afanya ziara ya kushtukiza Mariupol Ukraine na Crimea

ICC kazi kwao kumkamata, yupo Ukraine anavinjari mitaa ya mauripol

View attachment 2557853

===
Rais wa Urusi Vladimir Putin na Rais pendwa duniani ama mwamba wa dunia jana amefanya ziara ya kushtukiza katika rasi ya Crimea katika kuadhimisha miaka tisa tangu alipoinyakua kutoka Ukraine

Putin aliutembelea pia mji wa Ukraine wa Mariupol unaokaliwa kimabavu huku Mahakama ya wazungu wa ulaya magharibi wakibaki midomo wazi wasijue cha kumfanya.

Ziara ya Putin inajiri siku chache baada ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC kutoa waranti wa kukamatwa kwake kwa uhalifu wa kivita, ikimtuhumu kwa uwajibikaji katika utekaji nyara wa watoto nchini Ukraine.

Moscow imetupilia mbali uamuzi wa Mahakama hiyo. Kyiv inasema tangu kuanza kwa uvamizi huo Februari 2022, zaidi ya watoto 16,000 wa Ukraine walihamishwa kinyume cha sheria kuelekea Urusi. Wakati huo huo, mapigano makali yanaendelea huko Donetsk hasa katika mji wa Bakhmut.
Russia Federation....
 
Kuna vitu western media hawatakaa wakuoneshe. Nimeangalia hii video mpaka nikafarijika!!

Kweli hawa wananchi walionewa na utawala dhalimu wa Ukraine. Putin kawaokoa.

Link:
 
Kuna vitu western media hawatakaa wakuoneshe. Nimeangalia hii video mpaka nikafarijika!!

Kweli hawa wananchi walionewa na utawala dhalimu wa Ukraine. Putin kawaokoa.

Link:

Wewe unafarijika na mambo ya putin wakati sisi CCM tunakutendea makubwa hufarijiki.Au ndio ukoloni mamboleo,kila kitu wanachofanya wazungu wa urusi unafarijika.
 
Wewe unafarijika na mambo ya putin wakati sisi CCM tunakutendea makubwa hufarijiki.Au ndio ukoloni mamboleo,kila kitu wanachofanya wazungu wa urusi unafarijika.
Kuna kitu kinaitwa utu. Nnapoona binadamu mwenzangu ameokolewa kutoka kwenye udhalimu na wauaji lazima nifarijike. Pia nnapoona binadamu mwenzangu anaonewa kama jinsi ccm inavyotesa watanzania lazima nisikitike.
 
Kwahiyo KGB na Putin hawaui watu Ukraine msomi???

Back
Top Bottom