- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Rais wa Urusi, Vladimir Putin, ametoa kauli yenye utata kuhusu Afrika, akisema, “Afrika ni makaburi kwa Waafrika. Inawezekanaje makaburi yakastawi?”
Putin ameeleza kuwa Waafrika waliofanikiwa huweka fedha zao Uswisi, hupata matibabu Ufaransa, huwekeza Ujerumani, hununua bidhaa Dubai, hutumia bidhaa za Kichina, husali Roma au Mecca, watoto wao husoma Ulaya, na husafiri kwenda Canada, Marekani, na Ulaya kwa utalii. “Wanapofariki, huzikwa Afrika,” amesema Putin.
Putin ameeleza kuwa Waafrika waliofanikiwa huweka fedha zao Uswisi, hupata matibabu Ufaransa, huwekeza Ujerumani, hununua bidhaa Dubai, hutumia bidhaa za Kichina, husali Roma au Mecca, watoto wao husoma Ulaya, na husafiri kwenda Canada, Marekani, na Ulaya kwa utalii. “Wanapofariki, huzikwa Afrika,” amesema Putin.
- Tunachokijua
- Kumekuwepo na nukuu inayosambaa mtandaoni ikidaiwa kuwahi kuzungumzwa na Rais wa Urus, Vladimir Putin kuhusu bara la Afrika.
“Afrika ni makaburi kwa Waafrika. Inawezekanaje makaburi yakastawi? Waafrika waliofanikiwa huweka fedha zao Uswisi, hupata matibabu Ufaransa, huwekeza Ujerumani, hununua bidhaa Dubai, hutumia bidhaa za Kichina, husali Roma au Mecca, watoto wao husoma Ulaya, na husafiri kwenda Canada, Marekani, na Ulaya kwa utalii. “Wanapofariki, huzikwa Afrika,” amesema Putin.
Nukuu hii imekuwa ikisambaa mtandaoni kwa muda mrefu (hapa na hapa) na Agosti 6, 2024, baadhi ya kurasa za Mitandao ya kijamii nchini Tanzania ziliichapisha pia mtandaoni (Hapa)
Kauli hii imepokelewa kwa furaha na baadhi ya watu huku wakimsifu Putin kwa kusema ukweli kwani baadhi ya viongozi wamekuwa wanatumia vibaya madaraka yao.
Ukweli upoje?
Ufuatiliaji wa JamiiCheck haujapata chanzo chochote cha kuaminika kilichoandika kuhusiana na nukuu hii. Aidha, makavazi ya hotuba za Rais huyo hayana taarifa yoyote inayozungumzia kauli hii.
Katika utafutaji wake, JamiiCheck imebaini kauli hii inayohusishwa na Rais Putin iliwahi kuandikwa mtandaoni Novemba 28, 2018 ikitaja Nchi ya Pakistan kama kaburi la wananchi wake tofauti na Afrika kama inavyodaiwa sasa.
Taasisi zingine za uhakiki kama Reuters na AFP waliwahi pia kuikanusha nukuu hii.
Aidha, taasisi ya Observador inayopatikana nchini Urusi imewahi kuihakiki taarifa hii na kuuita ya uongo.
"Madai yanayohusishwa na Putin kwamba "Afrika ni makaburi ya Waafrika" ni ya uongo. Picha iliyoambatanishwa na chapisho hilo haioneshi mahali au tarehe ambapo rais wa Urusi angetoa taarifa kama hiyo. Kwa hivyo, kulingana na uhakiki wa Observador, habari sio sahihi" waliandika Observador.