Rais Putin asifia uhusiano wa karibu wa Urusi, China

Rais Putin asifia uhusiano wa karibu wa Urusi, China

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
365
Reaction score
1,374
PUTIN ASIFIA UHUSIANO WA KARIBU WA URUSI, CHINA

Rais wa Urusi, Vladmir Putin, leo ameyasifu mahusiano ya karibu ya nchi yake na China, katika mkutano na mwenzake wa China, Xi Jinping, kabla ya kufunguliwa kwa Michezo ya Olimpiki ya majira ya Baridi mjini Beijing.


Viongozi hao wawili wamekutana katika Mji Mkuu wa China wakati nchi zao zikilenga kuimarisha mahusiano huku zikikabiliwa na ongezeko la ukosoaji kutoka nchi za Magharibi.

Akizungumza kabla ya mkutano wao, Putin alisema Moscow imeandaa kandarasi mpya ya kusambaza gesi asilia ya mita za ujazo bilioni 10 nchini China kutoka Mashariki ya Mbali ya Urusi.

Baadaye leo, Rais huyo wa Urusi atashiriki katika sherehe za ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki.

Beijing na Moscow wamelaani hatua ya nchi kadhaa ya kuisusia kidiplomasia michezo hiyo zikilalamikia kile serikali za Magharibi zinahoji kuwa ni ukiukaji mkubwa wa haki nchini China.

Putin.jpg
 
Aah hiki ndo kimemfanya Putin atulie kwanza huko ukraine............acha wapeane airtime kuimba kupokelezana
 
Wanyama wamekutana ......nadhani dunia imebalance
 
Hakuna urafiki wa kweli Kati ya China na Urusi. Kinachowafanya URUS na China wawe pamoja Kama tunavyowaona hivi Sasa ni kwasababu wana adui mmoja TU, yaani Marekani. Siku Marekani ikianguka na kutokuwa tishio tena kwa China au URUS ndipo utajionea ninachokizungumza.
 
Putin akijifanya kusinzia wakati timu ya Ukraine ikiingia uwanjani katika sherehe ya ufunguzi wa Olympics.

1644070189975.png
 
Back
Top Bottom