Rais Ramaphosa ameapa kuwachukulia hatua waliomtorosha Nabii Bushiri kutoka Afrika Kusini kwenda Malawi

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2020
Posts
3,585
Reaction score
8,106
RAIS wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa amesema kuwa kutoroka kwa Nabii wa Malawi na mke wake nchini humo ni jambo ambalo analifuatilia kwa karibu na ameahidi kuchukua hatua baada ya kupata taarifa za kina.

Nabii Shepherd Bushiri na mke wake Mary, wanakabiliwa na mashtaka ya ulaghai na utakatishaji wa fedha nchini Afrika Kusini.

Wawili hao walitoroka nchini Afrika Kusini wiki liyopita na kujiwasilisha kwa polisi nchini Malawi baada ya Afrika Kusini kutoa kibali cha kukamatwa kwao.

Kupitia televisheni ya eneo, Rais Ramaphosa alisema tukio la wawili hao kutoroka “halikutakiwa kutokea”.

“Bila shaka tutachukua hatua,” Rais alijibu alipoulizwa ikiwa serikali inapanga kufanya lolote.

Baadhi ya taarifa zinasema kuwa muhubiri huyo aliyejitangaza mtume pamoja na mke wake walitoroshwa nchi humo kwa njia haramu na genge la watu ambalo linahusika na uuzaji wa magari yaliyoibwa nchini Afrika Kusini na kupelekwa Malawi.

Pia kuna baadhi ya vyombo vya habari Afrika Kusini vilivyosema kuwa nabii huyo alitoroka kwa kutumia ndege ya rais. Hata hivyo serikali zote mbili zimekanusha madai hayo.
 
Ngoma ikilia sana hupasuka! Kadanganya na kuibia watu kupitia imani na ss mwisho wake ndo huo. Kaanza kulialia kuwa anaonewa kasahau uongo na ushenzi alowatendea watu! Mauti ndo ynamkuta hivyo na arudishwe akabebe dhambi zake.
 
Mkiambiwa dini ni ujanja ujanja mnabisha 😂
Ujanja kila sehemu upo,hata huko mahospitalini na mahakamani nako kuna ujanja ujanja pia. Cha muhimu ni kuwa makini na hao wajanja wajanja.
 
Asilimia 99 ya watumishi Ni wajasiriamali( matapeli) wanaotumia ujinga wa watu kuwaibia.Kama bushiri angekuwa msafi asingetoroka na kamA angekuwa mtumishi was Mungu kweli asingeogopa kuithibitisha haki yake mbele ya wale wanaomwamini kwa kujitetea mahakamani. Huu Ni ufunuo dhahiri kwa wale mnaokimbilia miujiza kwa manabii na mitume kuwa mnaibiwa mchana kweupe someni maandiko mpate maarifa ya kumjua Mungu.
 
Watasomaje maandiko wakati wanapenda miujiza,nami nasema wengi ni matapeli

Sent from my itel A44 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom