Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Ni unafiki kwa mtu anayeamini dini moja kubwa na ya kale ya uongo kumsema mwingine anayeamini dini ndogo na mpya kuwa gaidi.Rais William Ruto wa Kenya, amemtangaza Mchungaji Paul Mackenzie Nthenge wa kanisa la Good News International Ministry kuwa GAIDI na kutaka ashtakiwe kwa makosa ya Ugaidi. Ruto amesema tuhuma zinazomkabili Mchungaji huyo zinaangukia kwenye sheria ya kuzuia ugaidi no.30 ya mwaka 2012 (Prevention of Terrorism Act, 2012).
Mackenzie anatuhumiwa kuwalazimisha waumini wake kufunga hadi kufa (Fasting to death) ili wapate ticket ya kuonana na Yesu ana kwa ana mbinguni. Mpaka sasa maiti 98 zimefukuliwa katika msitu wa Shakahola kaunti ya Kilifi, ambapo Mchungaji huyo anamiliki eneo lenye ukubwa wa ekari 800.
Baadhi ya maiti zimekutwa bila viungo, huku waumini waliookolewa hai, wakikataa kula na wengine wakakitaa kuondoka eneo hilo hadi walipoondolewa kwa nguvu na vyombo vya dola. Mchungaji Mackenzie anashikiliwa kwa upelelezi kabla ya kupandishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.!View attachment 2601474View attachment 2601475View attachment 2601476
Hizi dini zote zinazohubiri Mungu mkali anayechoma watu moto ni dini za ugaidi.
By the very definition of ugaidi.