Kenyan
JF-Expert Member
- Jun 7, 2012
- 414
- 314
Rais William Ruto amerejea nchini dakika chache zilizopita ambapo amepokelewa na Naibu wa Rais Rigathi Gachagua, Mkuu wa Jeshi la Ulinzi Robert Kibochi pamoja na Inspekta Jenerali wa polisi Japheth Koome.
Ruto ametokea nchini Ujerumani na Ubelgiji ambalo alikuwa amezuru kikazi na anatarajiwa kufanya mkutano juu ya Usalama wa raia na mali, kuelekea maandamano ya leo ya Upinzani ambayo tayari yameanza katika maeneo ya Kanda ya Ziwa huku kilele chake kikitarajiwa kuwa Jiji Kuu la Nairobi.
Tayari mamia ya maafisa wa polisi wameshika doria katika sehemu nyingi za Nairobi hasa Kibra, Mlango Kubwa, Mathare na maeneo mengine.