Rais William Ruto na Kiongozi wa Chama cha ODM, Oburu Oginga, wameongoza mkutano wa viongozi wa kisiasa unaohusishwa na mfumo wa Broad-Based Government mjini Naivasha, huku Kenya ikielekea kwenye uchaguzi mkuu wa 2027.
Mkutano huo unawaleta pamoja viongozi kutoka vyama vya UDA na ODM kwa ajili ya kujadili masuala ya kisiasa, utawala na mwelekeo wa ushirikiano wao kabla ya uchaguzi ujao.
Mazungumzo hayo yanatarajiwa pia kugusia utekelezaji wa makubaliano ya ushirikiano kati ya pande hizo mbili, pamoja na namna ya kuimarisha serikali ya Broad-Based.
Ushirikiano kati ya UDA na ODM ulianza kuchukua sura mpya baada ya Rais Ruto na aliyekuwa Kiongozi wa ODM, Raila Odinga, kuingia katika makubaliano ya kisiasa yaliyolenga kukuza utulivu na kushughulikia changamoto zinazowakabili Wakenya.
Hata hivyo, mkutano wa Naivasha unafanyika wakati ambapo tayari mjadala kuhusu uchaguzi wa 2027 umeanza kushika kasi. Vyama vya kisiasa vimeanza kujipanga, huku viongozi wakitathmini uwezekano wa miungano mipya na mikakati ya kushindana katika uchaguzi huo.
Kwa Ruto na Oburu, mkutano huo unatoa jukwaa muhimu la kutathmini hali ya kisiasa na mustakabali wa ushirikiano wa UDA na ODM.
Huku uchaguzi wa 2027 ukikaribia, macho sasa yanaelekezwa Naivasha kuona iwapo mkutano huo utaibua mwelekeo mpya wa siasa za Kenya.