Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Rais Ruto wa Kenya amesema hatoendelea kutoa ruzuku ya unga na badala yake atasaidia wakulima wadogo na wakubwa kufanya uzalishaji ambao utapunguza bei ya bidhaa hizo.
Bei ya unga nchini Kenya ilipanda sana kutokana na vita vya Ukraine na Urusi ambapo serikali chini ya Rais Uhuru Kenyata iliweka ruzuku ili kupunguza bei ya bidhaa hiyo inayotumika na wakenya wengi.
Rais Ruto ameenda tofauti na mtangulizi huku akiweka wazi kuwa ruzuku hizo zimekuwa zikiwagharimu wakenya fedha nyingi ambapo kila mwezi hutoa Ksh. Bilioni 7 ambapo kila mfuko wa unga ulilipiwa ruzuku ya Ksh. 100