Tunawauzia malighafi na wao hufaidika zaidi kwa mfano mahindi wao hutengeneza unga na kuuza somalia, ethiopia na sudani lakini pia pumba wanatengeneza vyakula vya mifugo au mahindi hayohayo wanapata mafuta ya kula, halafu mashudu ya Alizeti wao wakinunua kwetu wanayaprocess na kupata mafuta tena ya kula mengi tu na makapi wanafanya chakula cha mifugo, wananunua mbao mafinga na njombe na kwenda kuziprocess, haya asali ya sikonge wao hupata faida zaidi, kwahiyo kama alivosema mdau pale juu serikali yetu ichagize viwanda hata vidogo na vya kati ili tuuze bidhaa kamili kwenye hayo masoko lakini pia tutatengeneza ajira kwa wananchi wetu, lakini ukiuza malighafi ni sawa na Kuhamisha ajira za watanzania,