Rais Samia aachwe arekebishe nchi iliyokuwa katika sintofahamu

Rais Samia aachwe arekebishe nchi iliyokuwa katika sintofahamu

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
16,419
Reaction score
26,594
Siyo siri, nchi ilikuwa katika sintofahamu, hofu na ahadi ya ufukara kwa nchi na mtu mmoja mmoja.

Matokeo ya uongozi wa Mwendzake.

Kitu cha kwanza Mam Samia kaondoa ni hofu.

Hofu ilikuwa ya ya kutekwa, kubambikwa kesi za uhujuumu uchumi , kuuwawa na hata kuishia jela bila makosa yoyote.

Pili hofu ya ufukara.

TRA kutumika kupora mali za watu, uspotoa chako unabambikw uhujumu, kuibiwa na kunyang'anywa fedha kama BurueDe Change za Arusha.

Ukiwa mpinzani ndio kabisaa!

Kubambikwa kesi za madawa ya kulevya, kingi akiwa Makonda.

Kuuwa watu, kina Lwajabe na wengine kwenye visulfate.

Hivi vyoote Mama Samia anajaribu kuviondoa.

Kwa mwendo huu naamini hata Katiba Mpya haiko mbali sana.

Tusijaribu watanzania ku bite off more than we can chew.

Tukumbuke vibraka wa Mwendazake bado wapo, na wana madaraka.
 
Huwezi kujenga uchumi bila utawala bora na huwezi kuwa na utawala bora bila utawala wa sheria, na huwezi kuwa na utawala wa sheria kama hauheshimu haki za binadamu na uhuru wa mahakama! Na huwezi kupata yote haya bila katiba bora.Hii katiba ya sasa sio bora tunataka mpya!

E49_.jpg
 
Hakuna anayemzuia.

Tunataka tu atekeleze sheria ya mwaka 2012 ya mabadiliko ya katiba ili tupate katiba mpya.

Hii katiba anayotawala nayo kwa sasa inapingana na katiba ya Zanzibar ya mwaka 2010 kwenye mambo mengi na ya msingi. Sasa hatuwezi kuongoza nchi kwa katiba mbili zinazokinzana, lazima hili suala lifanyiwe kazi kuondoa discrepancy hii haraka sana
 
Wakati nchi inaingia kwenye sintofahamu yeye alikuwa ni mtendaji wa kata? acheni mambo ya ajabu, mikutano ya kisiasa inamzuia vipi kuamsha uchumi? kifupi ananufaika sn na hii katiba mbovu.
 
Maghufuli alidai anainyosha nchi we nae na mama ako mnataka mda wa kurekebisha, hakuna mwanadamu mwenye dhamana ya kurekebisha Taifa , huwa mnajidanganya tuu, endesha nchi Kwa mjibu wa taratibu na katiba
 
Hawezi kubali katiba mpya maana hii inampa utukufu sn
 
Maghufuli alidai anainyosha nchi we nae na mama ako mnataka mda wa kurekebisha, hakuna mwanadamu mwenye dhamana ya kurekebisha Taifa , huwa mnajidanganya tuu, endesha nchi Kwa mjibu wa taratibu na katiba
Well said
 
Wakati mwingine wanasiasa wanaweza kuwa ni sababu la anguko la taifa au ikawa sababu ya ustawi wa taifa, inategemea na nyakati husika.

Ni wananchi tu kuwa makini na ajenda za wanasiasa.
 
Wakati nchi inaingia kwenye sintofahamu yeye alikuwa ni mtendaji wa kata? acheni mambo ya ajabu, mikutano ya kisiasa inamzuia vipi kuamsha uchumi? kifupi ananufaika sn na hii katiba mbovu.
Mlipokuwa mnademka hapa mlikuwa hamjui haya?

Tulieni!

Hatutaki kelele zenu tunajenga nchi sisi
 
Back
Top Bottom