Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Akiwa nchini Cuba Rais Samia Suluhu Hassan ameeleza dhamira yake ya kuunganisha lugha ya Kiswahili na lugha ya Kihispaniola ambayo ni lugha ya pili kwa kuzungumzwa na watu wengi duniani baada ya lugha ya kiingereza
Lengo likiwa ni kuwaleta watu wengi pamoja, kuimarisha ushirikiano wa kibiashara, kiuchumi na kiutalii.
Hayo yameelezwa katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa la Kiswahili Novemba 8, 2024 jijini Havana Cuba ambayo ilieleza kuongeza fursa za ajira kwa vijana kupitia ukalimani kwenye mashirika mbalimbali ya kimataifa na hata kuandaa na kuuza machapisho, huku akisisitiza umuhimu wa Wananchi wa Cuba, Ukanda wa Caribean na Amerika ya Kusini kujifunza kiswahili ili watumie fursa zilizopo Tanzania na Afrika katika shughuli za kiuchumi.
“Tunaamini Kiswahili kitarahisisha na kuwezesha mawasiliano, kwa ajili ya mtangamano, biashara, utalii na uwekezaji barani Afrika kwakuwa kimekuwa na wazungumzaji wengi na kuwa lugha ya jumuiya mbalimbali za kikanda ikiwemo Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Umoja wa Afrika” amesisitiza Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Source: CFM Tanzania