Rais Samia aagiza mapitio ya tozo ili kupunguza gharama za bando

benzemah

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2014
Posts
1,533
Reaction score
3,187
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akizungumza katika kipindi cha Clouds360 kinachorushwa kupitia Clouds TV ameeleza kuwa Rais wa Tanzania; Dkt Samia Suluhu ameridhia kufanyika kwa mapitio ya baadhi ya tozo ili kupunguza gharama za Bando kama ambavyo watanzania wengi wamekuwa wakihimiza huku pia akieleza kuwa kuna mikakati zaidi ya kupunguza gharama za bando nchini ambayo itawekwa wazi siku za usoni.

“Mheshimiwa Rais amekubali tupitie baadhi ya tozo, ili kupunguza gharama za matumizi ya bando, na pia zipo hatua mbalimbali tunazichukua ambazo siku zijazo tutaweka wazi hatua hizo ambazo zitaleta unafuu katika gharama za matumizi ya intaneti.”
 
Nani aliziwwka hizo tozo
 
Government psyops. tunakaribia 2025 so beware of the propaganda. steps ni hizi: -
Step 1 : the government will create a problem
Step 2: it will then let the problem manifest itself
Step 3: They will then Show up as 'heroes' to solve the problem they created in the first place

Rinse and repeat mpka tupate Term II
 
Hivi watanzania wana shida na bundle!? Mbona kuna wakati nchii hii inatia AIBU hivi!??
 
Is this really the issue to come forward address the nation..

Au waandishi hawana vitu vya kuhoji!??
 
Serikali inaweza ongeza Tsh 100 kwenye gharama lakini wakati wa kupunguza hupunguza Tsh 7 na kujitangaza.
 
unapoweka bei ya MB moja eti ni kati ya Tsh 1 na Tsh 9 huo ni uhaini! yaan tigo wakiuza GB kwa 1,000 au 9,000 ni sawa tu! hapa ina maana Nape alikuwa anafanya makusudi au ni mpumbafu wa akili!


yaan ni sawa na kusema petrol iuzwe kati ya BUKU na BUKU TISA!

mweee aibu naiona mie
 
Hao ni mavii
 
Bladifaken, hawa usiwaamini
 
Janja ya nyani hiyo, wameona Lissu mikoani akigusia ishu ya bando wananchi wanamuelewa vizuri sana wameanza kuogopa.

Halafu wanajua uchaguzi wa serikali za mitaa upo kibarazani hapo mwaka 2024, ndo wanajifanya kupozapoza.
Jamaa wajanja sana lakini hatudanganyiki,
 
Unatengeneza tatizo, unapiga ndefu kisha unalitafutia ufumbuzi halafu unashangiliwa[emoji419][emoji375]
 
Una uhakika kuwa hatudanganyiki?
 
Mama akifanikiwa kukata gharama za internet kwa 50% atakumbukwa kwa hilo.
 

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…