Rais Samia aambiwe Makamu wa Rais ni Mkubwa kwa Rais wa Zanzibar, au anafanya makusudi!?

Hawa ndio wanadai katiba wakati iliyopo hawaielewi
Umenena vzur sana ,muungano huu hauna faida Kwa Wazanzibar kabsa ,,uvunjike hata kesho na pawe na sherehe kubwa ya kuagana ,na wakati tunaagana mafundi wetu wa umeme wawe pale wanakata umeme unafuliwa tz bara na kupelekwa Zanzibar,pia bara darsalam ,pwani na Dodoma tunajua jinsi Wazanzibar walivyonunua viwanja na kujenga siku ya kuvunja muungano pia Wazanzibar hao wawe wameondoa vyombo vyao kweny nyumba tajwa na kuwaachia watanganyika,viongoz ambao wapo bara wakifanya kazi wengine ni wakuu wa mikoa na wilaya huku Tanzania bara nao wawe tayar siku iyo ya sherehe ya kuagana ,chakula kinachotoka bara Mchele,mihogo ,mahindi navyo vitozwe Kodi kwenda Zanzibar kuanzia sku ya kuagana , na kakisiwa kenyewe hakana hata miaka 30 ijayo katamezwa na maji ili mfie huko shambash,,muungano hauna faida Kwa Wazanzibar,,,vunjeni kama kwel hauna faida
 
Ha ha haaaaa 🤣🤣🤣
 
Watanganyika tuwe makini na mwendo wa Mama.
Mkuu LOKASA chika, huyu ndie mkuu wa nchi, mkuu wa serikali na amiri jeshi mkuu, (head of nation, head of the government and CinC), the president is everything tuwe makini kivipi?. Civic education inahitajika sana kuwafundisha Watanzania, Rais wa JMT is an executive president. Je, wajua kuwa Rais wa JMT ndie Serikali, Bunge na Mahakama? Yuko juu ya Mihimili yote 3. Je, kuna uwezekano Rais wa JMT pia yuko juu Katiba?
Wazanzibar kibao wapo serikalini kwenye ofisi hata zisizo za Muungano na free wao kununua ardhi.
Hapa pia elimu ya uraia inahitajika kuwajilisha Watanzania kuwa Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye uraia mmoja tuu wa Tanzania na Watanzania wote wana haki sawa za Utanzania ikiwemo kumiliki mali, ardhi na ajira ndani ya JMT, ila Zanzibar ina utawala wake wa ndani, unaowahusu Wazanzibari pekee.
P
 
Na mama aachie Kasri lake la Mbweni
 
Unatakiwa ujue kwamba Makamu wa Rais si mjumbe wa baraza la Mawaziri! La pili ni kwamba ukubwa unapatokana kwa mamlaka na siyo jina la cheo ulichonacho, siyo kwa sababu mfano mtu anaitwa Rais wa chama cha wafuga nyuki eti ndo awe mkubwa kuliko mwenyekiti wa Halmashauri.
Rais wa Zanzibar ana mamlaka ya nchi ambayo ni mdau sawa kwa sawa wa Muungano! Tatu, Rus wa Zanzibar ana weza kubadilisha mipaka ya majimbo yote ya upande wa Znz, anateua ma RC wote wa upande ule,
Nne, Makamu wa Rais hana mamlaka ya kuteua hata mtendaji wa kata, anapataje ukubwa?
Makamu wa Rais anapanda hadhi pale tu anapotoka nje ya nchi ambapo Zanzibar inatambulika kama sehemu ya Tanzania.
 
Tatizo nani atamuuliza, yeye ni kiziwi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…