Rais Samia aambiwe Makamu wa Rais ni Mkubwa kwa Rais wa Zanzibar, au anafanya makusudi!?

Chato tumemalizana nao sasa bado Zanzibar
 
Kama serikali ya Zanzibar ipo na inatambulika.
Serikali ya Tanganyika ipo wapi?
 
Tatizo ni CCM. Huu upumbavu wote ulifanyiwa kazi kwenye rasimu ya Tume ya Jaji Warioba lakini maccm yaliukataa. Matatizo ya Muungano hayatakaa yaishe so long CCM iko madarakani.
 
Walivyoo kaa ndivyo angetambulusha hivyo alimua tu kupiga ukope tu haaa haa haa

Sent from my HUAWEI KII-L22 using JamiiForums mobile app
Kuna makosa kiprotocol na miaka hii 5 nadhani yatawekwa sawa. Ila haya matatizo yaliletwa na nyerere haya. Mana hapo mwanzo VP alitakiwa awe rais wa zanzibar na si vyenginevyo. Sasa sababu zake za kibinafsina maono yako hafifu ndo yameleta mtafaruku. Na ndo mana hutakuja kuona Tz historia inafundiswa kiuhalisia sababu ina kasoro nyingi
 
Alimruka Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Waziri wa Mambo ya Nje, akamtuma Rais wa Zanzibar kwenda kwenye kikao cha kimataifa Msumbiji.

Wakati mambo ya kimataifa ni mambo ya serikali ya muungano, si ya serikali ya Zanzibar.

Kuna kitu anataka kufanya.
 
Wekeni kwenye katiba sasa ili makamo wa raisi muungano awe ndio Raisi wa Tanzania Bara( Tanganyika) ili kuondoa utata kama ilivyokuwa zamani wakati wa Nyerere.

Kulikuwa na Raisi wa Zanzibar na andiye Makamu wa Raisi wa Muungano

Makamu wa pili wa raisi wa Muungano ambaye ndiye kiongozi wa serikali Tanganyika , na raisi wa Jamuhuri.
 
Kama serikali ya Zanzibar ipo na inatambulika.
Serikali ya Tanganyika ipo wapi?
Hili ndo la kujadili sasa na tukijadili hilo tunarudi kwenye katiba na umuhimu wa kupitiwa upya ili ikidhi haja na iendane na wakati. Hatuwezi tumia katiba ya 1977 sijui
 

Pia Rais wa Zanzibar ana nembo, mpambe (Aide de camp), bendera ya urais , ni mkuu wa nchi siku zote (sehemu mojawapo ya Muungano), ana majeshi ambapo huwateua yeye rais wa Zanzibar, kwa maana hiyo ki protokali Rais wa SMZ ni 'mkubwa' kuliko Makamu wa Rais wa Serikali ya Muungano



Toggle navigation
President's Office and Chairman of Revolutionary Council, Zanzibar

MEDIA » NEWS AND EVENTS​

Dk. Hussein Ali Mwinyi amewataka Makamanda wapya aliowateua waende wakajenge na kurudisha nidhamu katika vikosi hivyo​

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Commodore Azana Hassan Msingiri kuwa Mkuu wa Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo (KMKM) hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amewataka Makamanda wapya aliowateua kuwa Wakuu wa Vikosi Maalum vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,waende wakajenge na kurudisha nidhamu katika vikosi hivyo.Hafla hiyo ilifanyika Ikulu Jijini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo Makamo wa Kwanza wa Rais Othman Masoud, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid, Jaji Mkuu wa Zanzibar Othman Makungu, Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama, viongozi wa dini, watendaji wa Serikali na wanafamilia.
Alisema kwamba Jeshi ni nidhamu na ikikosekana nidhamu hakuna Jeshi, hivyo, nidhamu ilitetereka katika vikosi na ndipo alipoamua kuwachangua Makamanda hao ili walete uzoefu wao wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania.Rais Dk. Mwinyi alisema kuwa aliona haja na sababu ya kuwatumia Maafisa wa Jeshi la Ulinzi la Tanzania ili waweze kuiweka nidhamu katika vikosi vya SMZ.
Pia, Rais Dk. Mwinyi aliwataka kwenda kusimamia rasilimali zilizopo katika vikosi hivyo na taasisi walizopewa dhamana kwani kuna ubadhirifu mkubwa, wizi na mambo mengine ambayo hayapaswi kufanywa.Alisema kuwa Serikali imegundua kwamba wahasibu katika vikosi hivyo wanalipa mishahara ya watu ambao hawapo, wahasibu wanakata posho za askari ambapo pia, wanalipa mpaka watu ambao tayari washastaafu.
Alisema kwamba yeye mwenyewe amethibitisha hayo kwani hana nia ya kumuonea mtu, hivyo aliwataka wakuu hao wapya wa vikosi vya SMZ kuhakikisha wahasibu hawafanyi vitendo hivyo na kutaka yale mambo yasiofaa yote yawe basi.Rais Dk. Mwinyi alisema kwamba maduka ya vikosi yalikuwa yakitumika vibaya ambapo wahasibu hao walikuwa wakichukua mishahara ya askari kwa kisingizio cha makato ili ionekani walikuwa wamekopa halafu fedha zilikuwa zinakwenda kuchukuliwa madukani.
Alisema kwamba maduka hayo yanadhamira njema ya kuwasaidia maafisa na askari na isiwe vichochoro vya kupitisha fedha haramu.Katika suala zima la uzalishaji mali, Rais Dk. Mwinyi alisema kuwa wakati wa amani kazi ya vikosi vya ulinzi ni mafunzo na uzalishaji mali na kuvitaka vikosi hivyo vikajipange kupunguza ruzuku inayotoka Serikalini.
Hivyo, alivitaka vikosi kupunguza fedha zinazotoka Serikali zinazokwenda kwenye vikosi, ambapo awamu ya pili iwe kuondokana na ruzuku kwa kujitegemea na kutoa gawiwo kwa Serikali kwani vikosi hivyo vina fusra za kuzalisha mali.Rais Dk. Mwinyi alisema kwamba ndani ya vikosi kuna viwanda, kampuni ya ulinzi, mashamba, maeneo yanayofaa kwa utalii pamoja na chelezo na kueleza kwamba ipo haja ya chelezo kutumika kibiashara na kutaka kuhudumia meli mbali mbali zikiwemo zile za Zanzibar na nje ya Zanzibar.
Alivitaka vikosi kuingia kwenye ubia na watu wenye uwezo, alitaka mashamba yazalishe hasa ikizingatiwa kuwa uwezo huo upo na kutaka vikosi kuzalisha mali ili serikali ipunguze mzigo wa kubeba vikosi hivyo, huku akisisitiza kupatikana kwa haki kwa askari na maafisa sambamba na kupata stahili zao kwa wakati.Aidha, Rais Dk. Mwinyi alisema kwamba sio kama anapenda kufukuza watu wala hana nia ya kutafuta mchawi wala hana nia ya kufufua makaburi lakini pale mtu anapokuwa mbadhirifu, wizi wa mali ya umma wa fedha za Serikali hatonyamaza kimya na hilo litaendelea mpaka mambo hayo yakome.
Alisema kwamba ndio kwanza anaanza na nguvu bado hazijesha na kutoa mfano pale alipoivunja Bodi ya Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ), kutokana na ubadhirifu na kutoa angalizo kwa wengine.Rais Dk. Mwinyi alishangazwa na Bodi ya ZSSF kwa kufanya ubadhirifu na kusema kwamba kuanzia Januari hadi Machi Bodi hiyo imefanya vikao zaidi ya sita ndani ya miezi mitatu ambapo fedha zilizotumika ni TZS Milioni 99.7
“Najiuliza kulikuwa na dharura gani ya kufanya vikao sita ndani ya miezi mitatu…..kwa kawaida Bodi zinatakiwa kufanya vikao vinne kwa mwaka na ikitokea kuna dharura ndio wanaweza kukutana zaidi ya hapo lakini kuwe na dharura”, alisema Rais Dk. Mwinyi.Hivyo, Rais Dk. Mwinyi aliivunja Bodi hiyo na kusema kwamba hatosita wala kusimama kuvunja Bodi mpaka ubadhirifu wote uondoke.
Aidha, alisema kwamba wakati Serikali inajenga wapo watu wanaobomoa, na kusema kwamba wanaobomoa wakiwemo ndani ya Serikali na Taasisi nyengine mafanikio hayatopatikana na yeye ataendelea kupambana nao.Rais Dk. Mwinyi alitoa onyo kwa wengine na kusema kwamba yapo Mashirika ya Serikali hapa Zanzibar ambayo yanayopata faida ni machache sana na karibu yote ni hasara hivyo haiwezekani kuendelea na Bodi zenye hasara.
Aliwapongeza Wakuu wote wa Vikosi aliowaapisha hivi leo na kutaka wakafanye kazi kwa bidii na kuwataka askari na Maafisa wote wa vikosi vya SMZ kutokuwa na wasiwasi kwani lengo lake ni kujenga ili vikosi viwe madhubuti, vilivyowezeshwa na kuwa na mafunzo ya kutosha.Mapema Rais Dk. Mwinyi ambaye pia, ni Mkuu wa Vikosi hivyo kabla ya kuwaapisha Wakuu hao kwa mujibu wa Sheria aliwapaindisha vyeo vya Ukuu wa Vikosi hivyo ya SMZ.
Pia, alitumia fusra hiyo kumshukuru Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Venance Mabeyo pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi Kamanda Simon Siro kwa kukubali pendekezo lake la kuwateua Makamanda hao na kusisitiza kwamba yeye alikuwa na lengo la kutafuta viongozi na sio wataalamu kwani anachotaka ni viongozi na si fani zao.
Walioapishwa katika hafla hiyo ni Kanali Azana Hassan Msingiri kuwa Mkuu wa Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo (KMKM), Kanali Makame Abdallah Daima kuwa Mkuu wa Kikosi cha Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU), Kanali Rashid Mzee Abdallah kuwa Kamishna wa Kikosi cha Zimamoto na Ukozi.
Wengine ni Luteni Kanali Khamis Bakari Khamis kuwa Kamishna wa Vyuo vya Mafunzo, Luteni Kanali Burhani Zubeir Nassoro kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Uratibu na Udhibiti wa Dawa za Kulevya pamoja na ACP Ahmed Hamis Makarani kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi (ZAECA)

Source : Dk. Hussein Ali Mwinyi amewataka Makamanda wapya aliowateua waende wakajenge na kurudisha nidhamu katika vikosi hivyo | Presidents Office Zanzibar
 
Raisi wa zanzibar ni raisi wa nchi yenye mamlaka kamili. Na ndo anaunda jamhuri ya muungano wa Tanzania. Na sio jamhuri ya muungano wa tanganyika mbona mnakuwa wagumu kuelewa. Tanganyika imefinywa mamlaka na JMT.

Rais wa Zanzibar si amir jeshi mkuu,fahamu hilo kwanza,ukimaliza fahamu nchi moja kamwe haiwezi kuwa na marais wawili.Ndio maana Zanzibar hawana bunge wana baraza la wawakilishi.Zanzibar ni sehemu ya JMT ukiiondoa Zanzibar hakuna JMT.
 

RAIS SHEIN AJAJUU: "TUTAWASHA VIBATARI VYETU'!​

Tishio la John Magufuli lagonga mwamba kwa Rais wa Zanzibar
 
Ndiyo maana dhalim alifanya upendeleo wa wazi kupeleka kila kitu Chato kwani anajua kwa mamlaka na madaraka makubwa yanayokaribia ya Kimungu aliyo nayo hakuna wa kumuuliza. Muarobaoni wa sintofahamu hii uko kwenye rasimu ya Tume ya Jaji Warioba. Kiini cha mtanziko huu ni CCM kutanguliza uchama kwanza badala ya utaifa kwanza.
 
Hili la protokali wengi tumeliona mama ajulishwe makamu wa rais wa jamhuri ni juu ya rais wa zanzibar. Rais wa serikali ya zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi viko chini ya jamhuri ya muunguna. Hili la fedha sijasikia mgao kama ni sawa kwa sawa. Nadhani hiyo sawa itakua kulingana kila upande kwa uzito wa idadi ya watu.
 
Alimruka Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Waziri wa Mambo ya Nje, akamtuma Rais wa Zanzibar kwenda kwenye kikao cha kimataifa Msumbiji.

Wakati mambo ya kimataifa ni mambo ya serikali ya muungano, si ya serikali ya Zanzibar.

Kuna kitu anataka kufanya.
Kwa mara ya mwisho naelezea ili km hamtaki kuelewa.... rais samia ni raisi wa jamhuri ya muungano wa tanzania ambayo rais mwinyi ni mmoja wapo anaeunda jamhuri hiyo ya tanzania. Rais samia sio raisi wa jamhuri ya muungano wa tanganyika. Sijui umeelewa mantiki ya hiyo kitu
 
Hapo hakuna mjadala.
SERIKALI NI MOJA TUUU YA YA TANZANIA.
huo mkoa WA Zanzibar mkuu wake NI mkuu wa mkoa mwinyi
Hili ndo la kujadili sasa na tukijadili hilo tunarudi kwenye katiba na umuhimu wa kupitiwa upya ili ikidhi haja na iendane na wakati. Hatuwezi tumia katiba ya 1977 sijui
 
Kamuulize Nyerere ilikuwaje katiba ya Tanganyika ndo ikawa katiba ya Muungano? Halafu nyie hio ardhi yote bara haijakutosheni mpaka mje kutuchukulia na hichi kiardhi kidogo tulichonacho?

Kwa taarifa yako Rais wa Zanzibar ni mkubwa kuliko Makamo wa Rais.

Mliambiwa mueke serekali 3 mkakataaa sasa ndo mnajichanganya kama hivi. Kuna mambo mengi hayaingii akilini , huku zanzibar jimbo unaweza kulitembea kwa miguu kwa muda wa nusu saa tu, lakini lina mbunge na muwakilishi, mbunge ambae anakuja huko bara kuja kujadili mambo ya Tanganyika. Haiingii akilini ni kupoteza tu fedha za walipa kodi lakini serekali ya CCM haina hasara. Kwa nn hawa hawa wawakilishi wasikutane na wenzao wabara wakajadili mambo ya Muungano , na mambo ya Tanganyika waachiwe watanganyika wenyewe?
 
9 Mar 2017
Dr. Shein afoka Tishio la Rais wa serikali ya Muungano kuzima umeme Zanzibar bila kumuhusisha
Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein amesema serikali yake haitishiki na tishio la kukatiwa umeme na iko tayari kutumia vibatari na deni linalodaiwa sio la leo wa jana.


Magufuli aagiza Tanesco kuwakatia umeme wasiolipa Tanzania​

6 Machi 2017

Maelezo ya picha,
Rais Magufuli ameagiza Tanesco kuikatia umeme serikali ya Zanzaibar na wengine wote wanaodaiwa na Tanesco
Rais wa Tanzania John Magufuli jana aliiagiza kampuni ya ugavi wa umeme nchini humo (Tanesco) kuwakatia umeme wateja wote wenye madeni makubwa kwa kampuni hiyo, ikiwemo serikali ya Zanzibar, limeripoti gazeti la The Citizen.
Akizungumza kabla ya kuweka jiwe la msingi kwenye kituo kipya cha Tanesco mkoani Mtwara, rais Magufuli alisema kuwa tasisi zote za umma zinapaswa kulipa madeni la sivyo zitakatiwa umeme.
Alisema kuwa serikali ya Zanzibar pekee , kupitia shirika la umeme za Zanzibar (Zeco), ina deni la Tanesco kiasi cha shilingi bilioni 121 za Tanzania.
"Msiogope mnapaswa kukata huduma hii kwa taasisi yoyote ambayo hailipi bili zake.Nataka kumwambia waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo kwamba umeme unapaswa kukatwa hata Ikulu. Nikilala gizani, halafu maafisa wa Ikulu ambao hawajalipa watawajibika na sio wewe. Una hakikisho langu kwa hili.
Pesa za kulipa bili kawaida hutolewa kwa wizara zetu, lakini badala yake hupelkwa kwingine
."ninaambiwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar haijalipa Sh121 billion. Ninyi (Tanesco) si wanasiasa...mnapaswa kuzingatia majukumu yenu ya kitaaluma...kata huduma ya umeme.Nimesema hata kama ni Ikulu , polisi, jeshi ama shule , hakuna mwenye deni anaepaswa kuachwa . Ni kwa njia hii tu tunaweza kuhakikisha kwamba pesa zilizotengewa wizara kwa ajili ya umeme zinatumiwa kama ilivyopangwa ili Tanesco iweze kuendesha kazi zake na kushughulikia matatizo ya uhaba wa umeme. ''Tanesco haiwezi kuboresha huduma kwa sababu ya madeni ya serikali yasiyolipwa''.
Alipozungumza na gazeti la Citizen jana , Waziri wa nchi katika ofisi ya makamu wa pili wa rais , Bwana Mohammed Aboud, alisema kuwa mipango inafanyika kwa ajili ya kuliwezesha shirika la Zeco kulipa madeni ya Tanesco.
"Maagizo ya rais Magufuli yako wazi. Madeni lazima yalipwe na yatalipwa. Tumeanza mchakato wa kuhakikishwa suala hili linatatuliwa.Pia tumeiagiza Zeco kuacha kulimbikiza madeni mapya.
Mawaziri hao wawili walifanya mkutano juu ya suala hilo hivi karibuni na kujadili namna deni hilo linavyoweza kulipwa ," Bwana Aboud aliliambia gazeti la The Citizen
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…