PreGE2025 Rais Samia abubujikwa na machozi kwa salamu za kheri za Watanzania, aomba Umoja na Amani kwa Taifa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Rais Samia kupitia mitandao yake ya kijamii, amewashukuru wananchi kwa salamu nyingi za kheri na upendo walizozitoa katika kumbukizi ya miaka minne ya Kiapo cha kuitumikia nchi yetu katika nafasi ya Rais. Rais Samia alieleza furaha yake kwa kuwaona Watanzania wakimtakia mafanikio na ustawi wakati wa kuadhimisha kipindi hicho muhimu cha uongozi wake.

​

Katika ujumbe wake wa shukrani, Rais Samia amesisitiza umuhimu wa umoja, amani, na utulivu katika taifa. Alisema kuwa ni muhimu kwa Watanzania kuwa na mshikamano ili kuendeleza ustawi wa nchi na kuhakikisha maendeleo yanatimizwa kwa manufaa ya wote. Aliomba pia, kwa pamoja, tusali kwa Mwenyezi Mungu ili aendelee kuibariki Tanzania na kutuongoza katika utekelezaji wa majukumu yetu, kwa weledi na utu.

"Nawashukuru nyote kwa salamu nyingi za kheri na upendo katika kumbukizi ya miaka minne ya Kiapo cha kuitumikia nchi yetu katika nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Tuungane pamoja kumuomba Mwenyezi Mungu aendelee kuibariki nchi yetu, tudumu katika umoja, amani na utulivu. Tumuombe pia Mwenyezi Mungu aendelee kutuongoza katika utu na weledi kwenye utekelezaji wa majukumu yetu, na kuzibariki kazi tunazozifanya katika kuleta ustawi wa nchi yetu na Wananchi wote.

Kazi na Utu, Tunasonga Mbele."


​
 
Amekopa sana na haieleweki pesa inafanya miradi ipi mapya ukiacha ya jpm
 
Mwenyezi Mungu akujaalie afya njema na furaha mama wa taifa
 
Kuna wananchi wanalia zaidi kwa kudhulumiwa haki zao. Hili ndio muhimu sio show off ya naniliii naniliii
 
Mwenyezi Mungu tuokoe dhidi ya huyu Mama. Wape watanzania akili na mwongozo October wampe goodbye. Au wewe fanya kazi Yako.
 
Lucas Mwashambwa hatimae umekiwa kaka, boss amebubujikwa vibaya mno 🤣🤣🤣
 
Kwa hakika Rais Samia ni Mpango wa Mungu Mwenyewe. Taifa lina furaha sana mikononi Mwa Mama. Kila napokutana na watanzania naona namna nyuso zao zilivyo jaa tabasamu na matumaini makubwa.
 
Naona mmegoma kukumbuka miaka minne tangu kufariki kwa Jiwe 🐼
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…