Pre GE2025 Rais Samia achangia shilingi milioni 50, ujenzi wa shule ya Msingi na ujenzi wa majengo ya Zahanati inayomilikiwa na Bakwata Simiyu

Pre GE2025 Rais Samia achangia shilingi milioni 50, ujenzi wa shule ya Msingi na ujenzi wa majengo ya Zahanati inayomilikiwa na Bakwata Simiyu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Ndagullachrles

Senior Member
Joined
Jun 20, 2023
Posts
153
Reaction score
161
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amechangia kiasi cha shilingi milioni 50, katika harambee ya ujenzi wa shule ya msingi na uchangiaji wa majengo ya zahanati unamilikiwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania - BAKWATA mkoa wa Simiyu.

Harambee hiyo iliyoendeshwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI . Mohamed Mchengerwa imewezesha kupata fedha kwa shilingi milioni 150 ikiwa ni shilingi milioni 20 zaidi ya shilingi milioni 130 iliyolengwa.

Harambee hiyo imefanyika usiku wa Oktoba 12, 2024, katika adhimisho la Maulid ya Mkoa wa Simiyu kwa mwaka 2024, katika viwanja vya CCM wilayani Bariadi Mkoani Simiyu.

Katika harambee hiyo Waziri Mchengerwa aliyepewa heshima ya kuwa mgeni rasmi katika adhimisho hilo la siku takatifu ya kuzaliwa kwa mtume, amesisitiza umuhimu wa elimu dunia na elimu ya dini kwa jamii, akisema elimu ndiyo silaha na nuru ya kujikomboa dhidi ya majanga yote anayokabiliananayo mwanadamu Pamoja na kupata utukufu.

Kulikazia Waziri Mchengerwa ameiomba BAKWATA iweke miongozo itakayo wajenga waumini ili kutoa Uzalendo, maadili na kuipenda dini, watu na nchi yao, kuanzia ngazi ya awali, na kusisitiza jamii na wadau mbalimbali wausishwe, watoa mafunzo waanishwe na wajengewe uelewa na uwezowa maarifa na mbinu kwa maeneo ya vijijini na mjini.Alikadhalika Ameshauri kufanyika kwa mapitio yatakayokuja na maboresho ya mfumo wa elimu ya dini ya kiislam kwa marika makubwa na madogo ili kuweka ulinganifu wa mafunzo sahihi ya dini ya kiislam nchini.

“Utaratibu huo uguse kwa kina na upana, kijiografia katika maeneo ya vijijini hadi wasiofikika kwa urahisi na urahisi mjini, uandaliwe mpango mahususi wa biashara kwenye eneo hilo ili kushukuru ya madrasa na mifumo yake ya uendeshaji kwa vyanzo vya ndani vya rasiliamli za ainazote kwa kuwahusisha waumini ili kuweka utengamano sawia kati ya maeneo ya vijijini na mijini” alisema Waziri Mchengerwa.
Katika Harambee hiyo Waziri Mchengerwa amechangia kiasi cha shilingi milioni 10, huku Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akichangia shilingi milioni 50 na kufanya lengo lililokusudiwa awali la kukusanya shilingi milioni 130 kuvukwa hadi shilingi milioni 150.

Soma Pia: Bashungwa aongoza harambee ujenzi wa Ukumbi na Vyumba vya kulala Wageni Parokia ya Kasumo; zaidi ya milioni 45 zakusanywa


Awali Mufti mkuu wa Tanzania Sheikh Dkt. Abubakar Zuber miongoni mwa viongozi wakuu wa dini ya Kiislam walioshiriki katika Maulid hayo ameongoza dua ya kumshukuru na Kumwombea Rais Dkt. samia Suluhu Hassan, akiwataka waumini wote wa dini ya Kiislam kujitokeza kwenye orodha ya wapiga kura za mitaa, katika kipindi hiki ambapo Serikali inaendelea na zoezi hilo ili kuwapa sifa za kuwachagua viongozi wao katika uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba 27, 2024.
 
Back
Top Bottom