Rais Samia afanya Mkutano wa Hadhara, Ruangwa mjini, leo Septemba 18, 2023

Rais Samia afanya Mkutano wa Hadhara, Ruangwa mjini, leo Septemba 18, 2023

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi kwenye Mkutano wa Hadhara - Ruangwa Mini leo tarehe 18 Septemba, 2023.


Rais Samia amesema kuwepo Ruangwa ni mwendelezo wa ziara yake ya siku nne mkoani Lindi. Lengo la Serikali kutoa pembejeo na ruzuku ya mazao ni kuwajengea uwezo wa kutosha wakulima wa kujijenga, ili baadae waweze kununua wenyewe.

Nia ya Serikali ni kuifanya Ruangwa ifunguke kimaendeleo. Pia Serikali itajikita katika kufanya utafiti wa madini pamoja na kuwawezesha wachimbaji wadogo ili wachimbe vizuri.

Mradi mkubwa wa gesi wa LNG utakuwa manispaa ya Lindi, lakini faida zake zitakwenda Lindi nzima. Serikali ipo hatua za mwisho kujadiliana na wawekezaji na pindi makubaliano yatakafokiwa mradi huu utaanza rasmi.
 
Ila hawa jamaa.. kuna shida...look at their Facial Expressions
Screenshot_20230918-103142.jpg
 
Baada ya kugalagala hapo watajibiwa "tumelichukua, mkalitizame, kalishughulikieni, lifanyieni kazi, hii nchi ni kubwa tutalifikiria"
 
Kwahiyo haya magari yaliyotoka Songea na kujaza watu nayo yanaelekea Rwangwa ?
 
sasa ni ziara au mkutano wa hadhara? mambo ya mikutano awaachie vyama, serikali ifanye ziara kukagua maendeleo na kutatua changamoto, kama kutakuwa na wanachi basi anaweza zungumza nao, maana ikishaitwa mikutano tunashuhudia majungu na vijembe badala ya utatuzi wa matatizo
 
Back
Top Bottom