Rais Samia afanya uteuzi: Masauni aondolewa Wizara ya Mambo ya ndani, Kabudi apelekwa Wizara ya Habari na Michezo, Janabi kuwa mshauri wa Rais

Rais Samia afanya uteuzi: Masauni aondolewa Wizara ya Mambo ya ndani, Kabudi apelekwa Wizara ya Habari na Michezo, Janabi kuwa mshauri wa Rais

Wakuu,

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi na mabadiliko ya Viongozi mbalimbali.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, uteuzi na mabadiliko ya viongozi hao ni kama ifuatavyo:-

(i) Mhe. Rais Dkt. Samia amehamisha majukumu ya sekta ya habari kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwenda Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ambapo Mhe. Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo;

(ii) Mhe. Jerry William Silaa (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

(iii) Mhe. Dkt. Damas Daniel Ndumbaro (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria

(iv) Mhe. Mhandisi Hamad Yusuf Masauni (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira);

(v) Mhe. Dkt. Ashatu Kachwamba Kijaji (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi;

(vi) Mhe. Abdallah Hamis Ulega (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Ujenzi;

(vii) Mhe. Innocent Lugha Bashungwa (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi;

(viii) Bw. Gerson Msigwa ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali;

(ix) Dkt. James Henry Kilabuko ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu)

(x) Dkt. Stephen Justice Nindi ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo anayeshughulikia masuala ya ushirika na umwagiliaji;

(xi) Dkt. Suleiman Hassan Serera amehamishwa kutoka Wizara ya Kilimo kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda na Biashara.Aidha, Balozi Dkt. John Stephen Simbachawene atapangiwa kituo cha kazi;

(xii) Prof Mohamed Yakub Janabi ameteuliwa kuwa Mshauri wa Rais Masuala ya Afya na Tiba. Aidha, pamoja na nafasi hiyo Prof. Janabi ataendelea kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili

(xiii) Bw. Anderson Gukwi Mutatembwa ameteuliwa kuwa Balozi na atapangiwa kituo cha kazi;(xiv) Bw. Mobhare Matinyi ameteuliwa kuwa Balozi na atapangiwa kituo cha kazi;

(xv) Kamishna wa Polisi Zanzibar CP. Hamad Khamis Hamad ameteuliwa kuwa Balozi na atapangiwa kituo cha kazi;

(xvi) Kamishna wa Polisi CP. Suzan Kaganda ameteuliwa kuwa Balozi na atapangiwa kituo cha kazi;

(xvii) Bw. Thobias Makoba aliyekuwa Msemaji Mkuu wa Serikali ameteuliwa kuwa Balozi na atapangiwa kituo cha kazi.

Uapisho wa Viongozi walioteuliwa utafanyika Ikulu Ndogo, Tunguu Zanzibar tarehe 10 Desemba, 2024 kuanzia saa 5.00 asubuhi.


Afadhali matinyi ameteuliwa na kurudishwa kwenye game.
 
Huyo Atatupa Tabu Upande Wa Chakula
Utasikia "ili kupunguza kasi ya magonjwa yasiyoambukiza, nashauri bei ya sukari na mafuta ya kupikia iwe juu ili wananchi wajifunze kula visivyoungwa"

Mama: sawa sawa. (Anachukua simu anampigia waziri wa biashara) toa tamko kuadimika kwa sukari na mafuta nchini.

Wafanyabiasha: mafuta lita moja tsh elf 12. Sukari 1kg 7000. Nyama 1kg elf 17.

Raia: mmmhhh, hapo bora tule mboga za majani na uji usio na sukari. 😀😀
 
Suala la wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama kupewa nafasi za kisiasa linachochea sana uvunjifu wa amani wakati wa uchaguzi ili kuwafurahisha wanasiasa na kujipendekeza ili wapate uteuzi.
Rais aache kabisa kuwateua na awaache watumike kwenye majukumu yao ya msingi bila kujiingiza kwenye siasa.
 
Back
Top Bottom