Rais Samia afanya uteuzi: Masauni aondolewa Wizara ya Mambo ya ndani, Kabudi apelekwa Wizara ya Habari na Michezo, Janabi kuwa mshauri wa Rais

Rais Samia afanya uteuzi: Masauni aondolewa Wizara ya Mambo ya ndani, Kabudi apelekwa Wizara ya Habari na Michezo, Janabi kuwa mshauri wa Rais

Nilikuwa naiona ile orodha ya Madaktari 6 kwenye luninga wanaopendekezwa kugombea nafasi iliyoachwa Wazi kufuatia Kifo Cha Dr Ndugulile pale WHO Africa

Ni kama Janabi ameshawaacha wenzake nyuma

Baadae Mlale unono 😀
Acha kuli- abuse jukwaa na wanajf ati! Huyo Mollel wako na mzee wa nje ya box hebu wapeleke katika vituo vya afya huko kata za pembezoni wakajifunze! Nashangaa watu wanawaita madaktari.
 
Mama jiandae kushindia kijiko 1 cha wali kwa janaba sema jamaa yuko vizuri kwenye kushauri ila wabongo hatupendi ila angemupumzisha apewe kiti 1 muhimbili au mshauri
 
Wakuu,

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi na mabadiliko ya Viongozi mbalimbali.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, uteuzi na mabadiliko ya viongozi hao ni kama ifuatavyo:-

(i) Mhe. Rais Dkt. Samia amehamisha majukumu ya sekta ya habari kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwenda Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ambapo Mhe. Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo;

(ii) Mhe. Jerry William Silaa (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

(iii) Mhe. Dkt. Damas Daniel Ndumbaro (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria

(iv) Mhe. Mhandisi Hamad Yusuf Masauni (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira);

(v) Mhe. Dkt. Ashatu Kachwamba Kijaji (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi;

(vi) Mhe. Abdallah Hamis Ulega (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Ujenzi;

(vii) Mhe. Innocent Lugha Bashungwa (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi;

(viii) Bw. Gerson Msigwa ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali;

(ix) Dkt. James Henry Kilabuko ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu)

(x) Dkt. Stephen Justice Nindi ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo anayeshughulikia masuala ya ushirika na umwagiliaji;

(xi) Dkt. Suleiman Hassan Serera amehamishwa kutoka Wizara ya Kilimo kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda na Biashara.Aidha, Balozi Dkt. John Stephen Simbachawene atapangiwa kituo cha kazi;

(xii) Prof Mohamed Yakub Janabi ameteuliwa kuwa Mshauri wa Rais Masuala ya Afya na Tiba. Aidha, pamoja na nafasi hiyo Prof. Janabi ataendelea kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili

(xiii) Bw. Anderson Gukwi Mutatembwa ameteuliwa kuwa Balozi na atapangiwa kituo cha kazi;(xiv) Bw. Mobhare Matinyi ameteuliwa kuwa Balozi na atapangiwa kituo cha kazi;

(xv) Kamishna wa Polisi Zanzibar CP. Hamad Khamis Hamad ameteuliwa kuwa Balozi na atapangiwa kituo cha kazi;

(xvi) Kamishna wa Polisi CP. Suzan Kaganda ameteuliwa kuwa Balozi na atapangiwa kituo cha kazi;

(xvii) Bw. Thobias Makoba aliyekuwa Msemaji Mkuu wa Serikali ameteuliwa kuwa Balozi na atapangiwa kituo cha kazi.

Uapisho wa Viongozi walioteuliwa utafanyika Ikulu Ndogo, Tunguu Zanzibar tarehe 10 Desemba, 2024 kuanzia saa 5.00 asubuhi.


Hivi tangu Machi 2021, teuzi zimefanyika mara ngapi? Ni sawa na teuzi mara ngapi kwa mwezi?
 
kulikoni suzan kaganda, hakyamungu wanaume haki zetu zinaenda potea, si ndo alisema tukinyimwa twende kwake au?
 
Sasa hivi ni zamu ya Polis na watendaji kata kutumbua tu. Hao kwa sasa ni miungu watu
 
Yule aliyemuoa mtangazaji clouds fm yuko wapi?? Mbona kama mkeka umechanika tayar ?
 
Kuhusu kabudi hiyo wizara anaiweza, anajua mengi yanayorandana na wizara hiyo licha ya taaluma yake ya uanasheria, usanii na habari anaweza
 
Tutegemee kuona Rais akikonda au hata kufa Kwa njaa,
Kamteua Janabi awe mshauri wa mambo ya Afya, soon atazuiliwa kula na kupata juu maana kutasababisha moyo utanuke
 
Kila nikimuangalia Bashungwa namuona kafanana na watu wa nchi jirani wale wachokozi wachokozi.😁
 
Back
Top Bottom