Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,067
- 10,938
Rais Samia afanya uteuzi na kufanya mabadiliko ya watendaji wa Serikali.
---
Zuhura Yunus, aliyekuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, na Felister Mdemu, aliyekuwa msaidizi wa Rais katika Maendeleo ya Jamii, ni miongoni mwa viongozi walioteuliwa kushika nafasi mpya. Petro Itozya, aliyekuwa msaidizi wa Rais katika masuala ya siasa, na Nehemia Mandia, aliyekuwa msaidizi wa Rais upande wa sheria, pia wamepata nafasi mpya za uongozi.
Katika uteuzi wake, Rais Samia amemteua Stanslaus Nyongo kuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Mipango na Uwekezaji. Zuhura Yunus ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), huku Felister Mdemu akiteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu.
Amon Mpanju naye ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu akishughulikia masuala ya maendeleo ya jamii.
Petro Itozya ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, wakati Fatma Nyangasa amehamishwa kutoka Kisarawe kwenda Kondoa. Dk. Hamis Mkanachi amehamishwa kutoka Kondoa kwenda Urambo, akichukua nafasi ya Elibariki Bajuta, ambaye atapangiwa majukumu mengine.
Katika mabadiliko mengine, Reuben Chongolo amehamishwa kutoka Wilaya ya Songwe kwenda Mufindi, huku Frank Sichwale akihamishwa kutoka Mufindi kwenda Songwe.
Kwa upande wa wakurugenzi, Mussa Kitungi ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia, Kalekwa Kasanga kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, na Shaaban Mpendu kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Babati. Sigilinda Mdemu ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele.
Milton Lupa ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo, huku Upendo Mangali akihamishwa kutoka Halmashauri ya Mji wa Babati kwenda Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga. Kisena Mabuba amehamishwa kwenda Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma, na Teresia Irafay amehamishwa kwenda Halmashauri ya Wilaya ya Hanang'.
Rais Samia pia ameteua majaji wapya wa Mahakama Kuu ya Tanzania. Nehemia Mandia ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Projestus Kahyoza na Mariam Omary pia wameteuliwa kushika nafasi za majaji wa Mahakama Kuu.
Uapisho wa Naibu Waziri, Naibu Makatibu Wakuu, na Majaji wa Mahakama Kuu utafanyika kwa tarehe itakayopangwa baadaye.
Pia, soma: Rais Samia Suluhu Hassan afanya uteuzi wake wa kwanza Ikulu. Gerson Msigwa atolewa Ikulu, Dotto James ahamishwa. TPA, TCRA na TRA zapata wakuu wapya