Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya mabadiliko katika safu ya uongozi kwa kuwahamisha wakuu wa wilaya wawili na kuteua viongozi wapya kwenye nyadhifa mbalimbali.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, mabadiliko hayo ni kama ifuatavyo:
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, mabadiliko hayo ni kama ifuatavyo:
Wakuu wa Wilaya waliohamishwa:
- Dkt. Vicent Naano Anney - Kutoka Wilaya ya Bunda kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Maswa.
- Aswege Enock Kaminyoge - Kutoka Wilaya ya Maswa kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Bunda.
Walioteuliwa kuwa wenyeviti wa bodi mbalimbali:
- CPA Juma Ajuang Kimori - Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO), akichukua nafasi ya Bw. Yona Killagane.
- Prof. Edward Gamaya Hoseah - Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Benjamin Mkapa, akichukua nafasi ya Dkt. Deo Mtasiwa.
- Bi Renatha Mtunda Rugarabamu - Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), akichukua nafasi ya Bw. Emmanuel Humba.
- Jaji Mstaafu Awadh Mohammed Bawazir - Mwenyekiti wa Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA), akichukua nafasi ya Jaji Mstaafu Sauda Mjasiri.
- Balozi Ramadhani Muombwa Mwinyi - Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa, akichukua nafasi ya Dkt. Salim Ahmed Salim kwa kipindi cha pili.