Pre GE2025 Rais Samia Afanyiwa Maombi Mazito Mkoani Simiyu

Pre GE2025 Rais Samia Afanyiwa Maombi Mazito Mkoani Simiyu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Ndugu zangu Watanzania,

Kinachopatikana kwa Maombi hulindwa kwa Maombi. Rais wetu mpendwa Amefika hapo alipo kiuongozi kwa Neema tu ya Mwenyezi Mungu. Amepanda na kukwea ngazi za kiuongozi kwa Msaada Wa Mungu Mwenyewe,ameruka viunzi na kuvushwa katika mitihani ya kila aina kwa Neema ya Mungu.

Amepita katika milima na mabonde ya kiuongozi na kufanikiwa kuvuka kwa Neema ya Mungu. Ndio Maana amekuwa mtu mwenye hofu ya Mungu na Mcha Mungu. Ndio sababu amekuwa mwenye kumtumaini Mungu kwa kila jambo. Ndio maana wakati wote anaomba Neema ya Mungu kumuongoza .

Ndio sababu hata viongozi wa Dini wamekuwa karibu sana na Rais wetu Mpendwa na kumuombea sana wakati wote. Ndio maana Makanisani na misikitini unaona watu wakipiga magoti na kujinyenyekeza mbela za Mungu kwa ajili ya kumuombea Rais wetu kipenzi .

Sasa katika kuendelea na utamaduni huo Mkoani Simiyu mamia kwa maelfu ya wananchi wamefanya maombi maalumu ya kumuombea Rais wetu Mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan Mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia, simba wa nyika, komandoo wa vita, nyota ya matumaini na nuru ya wanyonge.

Hii ni katika Kumuomba Mungu aendelee kumlinda,kumtetea na kumpigania Wakati wote Rais wetu. Ni katika kuhitaji msaada wa Mwenyezi Mungu katika ulinzi wa Rais wetu ambaye ndiye mtoa njia na maarifa kwa Mwanadamu.
Screenshot_20250217-213345_1.jpg


Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Back
Top Bottom